Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maguire achimba mkwara Man United

Harry Maguire After Man Utd Concede A Goal Harry Maguire

Thu, 12 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Beki wa kati wa Manchester United, Harry Maguire amedai kuwa kama ataendelea kupata nafasi ndogo ya kucheza chini ya ‘Kocha’ Erik ten Hag basi atafikiria kuondoka ifikapo Januari 2024.

Maguire ambaye alitoa 'asisti' ya ‘goli’ la ushindi ‘mechi’ iliyopita dhidi ya Brentford, amesema kuwa hawezi kubaki ‘klabuni’ hapo akiwa anacheza mara moja kila mwezi na hali hiyo ikiendelea kuwa hivyo atazungumza na ‘klabu’ hiyo kwa sababu anaamini uwezo wake na anataka kuonesha ili awe sehemu ya wachezaji muhimu katika ‘timu’ hiyo.

Ikumbukwe Maguire awali alikuwa nafasi ya kuanza katika kikosi cha kwanza kutokana na walinzi wa Man United kuwa majeruhi, wakiwemo Rafael Varane, Lisandro Martinez, Aaron Wan-Bissaka, Tyrell Malacia, Luke Shaw na Sergio Reguilon.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live