Beki wa zamani wa Manchester United, Patrice Evra amefichua jinsi mkutano wake na Sir Alex Ferguson ulivyomshawishi kuchagua kujiunga na United badala ya Liverpool mnamo 2006.
Mfaransa huyo amepata hadhi ya kuwa mmoja wa magwiji wa muda wote wa United baada ya kushinda mataji matano ya Ligi Kuu, matatu ya Kombe la Ligi na Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa muda wa miaka minane alipokuwa Old Trafford.
Evra sasa amefichua mazungumzo aliyofanya na Ferguson katika uwanja wa ndege huko Paris yalimpelekea kujiunga na United “Sir Alex alizungumza na wakala wangu na tukakutana katika uwanja wa ndege wa Charles de Gaulle mjini Paris.
Hakuzungumza Kifaransa kwa hiyo ilikuwa zaidi David Gill, wakala wangu alikuwa akitafsiri, lakini nakumbuka alikuwa akiuliza maswali kama, unakunywa? Hapana”
“Kabla ya United kuja wakala wangu alisema tuna Liverpool, Inter Milan na United. Nakumbuka wakala wangu alifurahi sana na kusema ‘Patrice ni Manchester United. Nilikuwa nikiitazama United kwa sababu ya Eric Cantona, ushawishi mkubwa”alisema Evra.
Evra uligeuka kuwa muhimu na mafanikio ya United kwani alikua mmoja wa mabeki wa pembeni bora zaidi duniani wakati alipokuwa akicheza hata hivyo, Ferguson alipoamua kustaafu uongozi mwaka wa 2013, iliashiria mwisho wa Evra, United na alidumu msimu mmoja tu chini ya David Moyes kabla ya kuondoka.
Mfaransa huyo alikwenda kujiunga na wababe wa Serie A, Juventus ambapo alishinda mataji matatu ya ligi ya Italia na vikombe viwili vya Italia na baadae alirejea Ufaransa akiwa na Marseille kabla ya kurejea England kwa mara pili akajiunga na klabu ya West Ham kabla ya kustaafu rasmi mwaka 2019.