Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maelfu ya mashabiki walikuwa na tiketi feki Fainali ya Madrid na Liverpool

Mashabiki Mkl Maelfu ya mashabiki walikuwa na tiketi feki Fainali ya Madrid na Liverpool

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Waziri wa Michezo wa Ufaransa, Amelie Oudea-Castera amesema kuwa Mashabiki waliokuwa hawana tiketi walisababisha vurugu za mwanzo katika fainali za Ligi ya Mabingwa Jijini Paris.

Waziri huyo ameongeza kuwa Mashabiki wengine waliokuwa na tiketi feki na waliokuwa wakilazimisha kuingia uwanjani waliongeza ukubwa wa fujo siku hiyo.

Polisi nchini Ufaransa wameshutumiwa kwa kurusha mabomu ya machozi na kupulizia vitu vyenye kuwasha (pepper spray) kwa baadhi ya mashabiki wa Liverpool wakati walipokuwa wakingojea kuingia uwanjani Jumamosi jioni.

Jana Jumatatu, Waziri wa Michezo, UEFA, Shirikisho la soka la Ufaransa, maafisa wa uwanja wa Stade de France na maafisa wa Polisi walikutana kujadili na kufanya tathmini ya yote yaliyotokea siku ya mechi hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live