Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid yawang’ang’ania Trent Alexander, Mac Allister

Trent X Mac Alister Madrid yawang’ang’ania Trent Alexander, Mac Allister

Sun, 19 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Baada ya kuhusishwa na Trent Alexander Arnold, vigogo wa Real Madrid wamehamia kwa mchezaji mwingine wa Liverpool, kiungo Alexis Mac Allister na wote imepanga kuwasajili dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Licha ya ripoti kudai hawajawasilisha ofa yoyote kwa ajili ya wachezaji hao, inaelezwa ofa hizo wanaweza kuwasilisha baada ya msimu kumalizika,

Madrid inamtaka staa huyu ili iboreshe eneo lao la kiungo ambalo ndani ya misimu miwili ijayo linaweza kuondokewa na mastaa kama Luka Modric na Toni Kroos.

Kwa upande wa Trent wanataka kumchukua kwa ajili ya maboresho kwenye eneo lao la ulinzi na imekuwa ikivutiwa na kiwango alichoonyesha kwa muda mrefu.

Tangu kuanza kwa msimu huu Alexis amecheza mechi 45 za michuano yote na kutoa asisti saba, wakati Trent akicheza mechi 36 za michuano yote na kutoa asisti tisa.

ASTON Villa imeonyesha nia ya kutaka kumsajili kiungo wa Chelsea na England, Conor Gallagher, 24, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi na imepanga kumtumia mshambuliaji wao raia wa Colombia, Jhon Duran, 20, kama sehemu ya ofa. Conor mwenye umri wa miaka 24, mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025. Mwenyewe ameonyesha nia ya kutaka kuendelea kusalia Chelsea.

MSHAMBULIAJI wa Brentford, Ivan Toney, 28, anatakiwa na Tottenham ambayo imepanga kusajili washambuliaji wawili dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Toney ambaye mkataba wake wa sasa unamalizika mwaka 2025, msimu huu amecheza mechi 16 za michuano yote na kufunga mabao manne. Arsenal na Chelsea pia zinamtaka nyota huyu na zinakabana koo kuhakikisha zinaipata saini yake.

MANCHESTER City na Tottenham zimeungana na Manchester United kuiwania saini ya beki wa Everton, Jarrad Branthwaite, 21, dirisha lijalo la majira ya kiangazi na mkataba wa staa huyo utakuwa umebakisha miaka mitatu kabla ya kumalizika. Everton inadaiwa kuhitaji zaidi ya Pauni 50 milioni ili kumuuza beki huyu ambaye msimu uliopita amecheza mechi 44 za michuano yote.

MANCHESTER United imeziambia Juventus, Napoli na Atletico Madrid wapo tayari kumuuza Mason Greenwood lakini kwa timu itakayotoa ofa nzuri kuliko nyingine. Greenwood mwenye umri wa miaka 22, kwa sasa anacheza kwa mkopo Getafe na mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2025. Mwenyewe hataki kurudi Old Trafford msimu ujao.

ANAYETAJWA kuwa kocha mpya wa Liverpool, Arne Slot inadaiwa kuwasilisha jina la beki wa Benfica, Antonio Silva kama mmoja wa mastaa anaohitaji wasajiliwe dirisha lijalo ili kuboresha zaidi timu hiyo hususani eneo la ulinzi. Silva mwenye umri wa miaka 20, ni mchezaji tegemeo katika kikosi cha kwanza cha Benfica na msimu huu amecheza mechi 57 za michuano yote.

RB Leipzig inahitaji Pauni 56 milioni kutoka kwa timu zinazomhitaji mshambuliaji wa timu hiyo, Benjamin Sesko na amekuwa akihusishwa na Arsenal iliyopanga kumsajili katika dirisha lijalo. Benjamin mwenye umri wa miaka 20, mkataba wake unamalizika mwaka 2028. Msimu huu amecheza mechi 42 za michuano yote na kufunga mabao 18.

ASTON Villa inataka kuwasilisha ofa kwenda Atletico Madrid ili kuipata saini ya beki wa timu hiyo, Mario Hermoso, 28, dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Hermoso ni mmoja kati ya mastaa wa Atletico walioonyesha kiwango bora kwa msimu huu na amecheza mechi 41 za michuano yote. Mkataba wake unamalizika mwisho wa msimu.

Chanzo: Mwanaspoti