Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid yapepea, Barca yaja mdogomdogo

Dsd Mad Madrid yapepea, Barca yaja mdogomdogo

Tue, 19 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mambo yamekuwa moto kabisa huko kwenye La Liga. Real Madrid imeonekana kuwa siriazi kwenye mbio za ubingwa baada kushinda mechi zake na kujiimarisha kileleni kwenye msimamo wa ligi hiyo, lakini Barcelona wakionyesha kwamba sasa wamejipata na wapo tayari kwa vita.

Mchakamchaka wa La Liga ulianzia Ijumaa, ambapo Real Sociedad ilikuwa nyumbani kukipiga na Cadiz. Katika mchezo huo, Real Sociedad ilitumia vyema nafasi yake ya kucheza nyumbani baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 2-0, shukrani kwa mabao ya Merino na Zakharyan na kukusanya pointi zote tatu.

Ushindi unaifanya Sociedad kujenga mizizi kwenye nafasi ya sita katika msimamo wa La Liga na hivyo kuwa na uhakika wa kucheza Europa League msimu ujao, ambapo vita hiyo anachuana na miamba Betis na Valencia.

REAL MADRID HAIPOI Katika kipute kilichofanyika Osasuna, Real Madrid ilionyesha kwamba msimu huu inachokitaka ni kunyakua tu taji la La Liga baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 4-2.

Vinicius Junior, staa matata kabisa wa Real Madrid alikuwa kwenye kiwango bora na kuisogeza timu yake karibu kabisa na ubingwa wa msimu huu. Mbrazili huyo aliifungia Madrid bao la kuongoza kwenye dakika ya nne tu na baada ya hapo aliendelea kuwa mwiba mchungu kwa mabeki wa Osasuna.

Lakini, Osasuna si watu wa kukubali kushindwa kirahisi, walipambana na Ante Budimir akasawazisha bao mapema tu. Hata hivyo, Real Madrid ilikuwa na ubora zaidi, ambapo Dani Carvajal na Brahim Diaz walifunga kuiongezea mabao timu yao.

Osasuna ilifunga bao jingine katika dakika za mwisho, lakini ni Real Madrid walioondoka na pointi zote tatu ambazo zinawafanya kufikisha pointi 72, pointi nane zaidi ya timu inayoshika nafasi ya pili kwenye msimamo, Barcelona.

Mechi nyingine zilizopigwa Jumamosi, Mallorca iliikandamiza Granada 1-0, wakati Getafe ilitoka kifua mbele dhidi ya Girona kwa kuichapa bao 1-0, huku Athletic Bilbao ilishinda 2-0 dhidi ya Alaves..

BARCA GARI LIMEWAKA Barcelona ilionekana kuwa siriazi kwenye mbio za ubingwa, ikijaribu kuifukuzia Real Madrid kimyakimya ikiamini chochote kinaweza kutokea. Hadi sasa zimechezwa mechi 29, bado mechi tisa mbele, sawa na pointi 27, huku pengo la pointi baina ya timu hizo mbili ni nane tu.

Na kuonyesha kwamba wapo kwenye mbio, Barca ilipata ushindi mbele ya timu ngumu kabisa, Atletico Madrid na ilikwenda kuwafunga kwao, Wanda Metropolitano kwa mabao 3-0.

Kipigo hicho kilikuwa kizito sana kwa Atletico, ambapo mara ya mwisho kufungwa kama hivyo, ilikuwa Novemba 2016, walipofungwa 3-0 pia nyumbani.

Kipigo hicho kwa Atletico kilihitimisha mechi 25 bila ya kupoteza kwenye uwanja wa nyumbani, lakini Barca wao wakipata matumaini ya walau kwenda kujaribu kutetea ubingwa wao.

Mabao ya Joao Felix, aliyeiadhibu timu yake ya zamani na yale ya Robert Lewandowski na Fermin Lopez yalitosha kuifanya Barca kupata na ushindi huo mtamu kabisa ugenini.

Mechi nyingine zilizochezwa Jumapili, Rayo Vallecano iliichapa Real Betis 2-0, Villarreal ilikung’uta Valencia 1-0 na Celta Vigo waliipiga Sevilla 2-1.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live