Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid yalazimishwa sare na Elche

Real Elche Mchezo ulimalizika kwa sare ya magoli 2-2

Mon, 24 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vinara wa Ligi Kuu nchini Hispania La Liga Real Madrid wamelazimika kutokea nyuma kwa goli 2 na kutoa sare ya 2-2 na Elche katika mchezo wa Ligi hiyo uliopigwa Jumapili.

Mabao wa mapema ya Elche yametupiwa na Lucas Boye na Pere Milla lakini tuta la baadaye la kiungo mshambuliaji Luka Modric na goli la mlinzi Eder Militao yametosha timu hizo kugawana pointi kibabe.

Licha ya furaha ya alama moja, hofu kwa kocha Carlo Ancelotti ni kumpoteza mshambuliaji wake Karim Benzema ambaye alitolewa nje ya uwanja kutokana na majeruhi ingawa alikuwa ameshakosa tuta.

Mshambuliaji huyo wa kimataifa amefunga goli 27 katika mechi 33 msimu huu ikiwa moja ya fomu nzuri kabisa.

Sare hiyo inaendeleza utofauti wa alama nne baina ya timu iliyonafasi ya pili Sevilla ambao walitoa sare ya goli 2-2 na Celta Vigo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live