Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid yaisubiri Bayern dili la Alphonso Davies

Alphonso Davies Sad Alphonso Davies

Mon, 10 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Beki wa pembeni wa Bayern Munich, Alphonso Davies bado ameendele kuwa kwenye orodha ya wachezaji wanaowindwa na Real Madrid, ikihitaji huduma yake kwenye dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi huko Ulaya.

Davies, 23, bado hajaongeza mkataba mpya kwenye kikosi cha miamba hiyo ya Allianz Arena jambo linalozidi kuchochea ripoti za kwamba huenda aakamua kuachana na timu hiyo katika dirisha hili.

Hata hivyo, mabosi wa Bayern Munich bado hawajata tamaa kwenye mpango wao wa kumshawishi Davies kusaini mkataba mpya na kuendelea kubaki kwenye kikosi chao kwa muda mrefu.

Mkataba wa sasa wa Davies utafikia kikomo mwaka 2025, hivyo Bayern Munich haitaki kujiweka kwenye hatari ya kumpoteza bure mchezaji huyo mwakani.

Los Blancos imeripotiwa kuhitaji sana saini yake na mwanzoni mwa mwaka huu, wawakilishi wake walifanya mazungumzo na mabosi wa Bernabeu kuweka mipango sawa.

Na kinachoripotiwa kwasasa ni kwamba kinachosubiriwa ni Bayern Munich kama itafanikiwa kumshawishi asaini mkataba mpya katika majira haya na kama hilo likishindikana, basi kunaweza kuwapo kwa shinikizo la kumuuza ili wababe hao wa Allianz Arena wapate chochote kitu kuliko kusubiri mwakani aondoke bure.

Chanzo: Mwanaspoti