Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid yaichapa Barca ugenini, Atletico yalazimishwa sare

Alaba.jpeg Mfungaji wa bao la kwanza la Real Madrid, David Alaba

Mon, 25 Oct 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Barcelona wamekubali kichapo cha mabao 2-1 kutoka kwa mahasimu wao, Real Madrid katika mchezo wa La Liga siku ya Jumapili katika Uwanja wa Camp Nou, Barcelona.

Mabao ya Real Madrid yamefungwa na David Alaba dakika ya 32 akimalizia pasi ya Rodrygo na Lucas Vázquez dakika ya 90, dakika nne kabla ya Sergio Agüero kuifungia Barca la kufutia machozi katika muda wa ziada.

Real Madrid inafikisha pointi 20 na kupanda kileleni mwa La Liga ikizizidi wastani wa mabao tu Sevilla na Real Sociedad, wakati Barcelona inabaki na pointi zake 15 katika nafasi ya nane baada ya timu zote kucheza mechi tisa.

Vigogo wengine wa La Liga vijana wa Diego Simeone, wamelazimisha sare ya mabao 2-2 na Real Sociedad katika dimba la Wanda Metropolitano.

Magoli ya Atletico yamefungwa na Luis Suarez huku yale ya Real Sociedad yakiwekwa wavuni na A. Soerloth 7' na A. Isak 48'.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live