Klqbu ya Real Madrid ya Uhispania imefabikiwa kutinga hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Barani Ulaya (UEFA Champions League) baada ya kuikanda Chelsea (wenyeji wa mchezo) ya Uingereza kwa bao 2-0 usiku wa kuamkia leo.
Mabao yote ya Madrid ambao ni mabingwa watetezi wa kombe hilo yamefungwa na Rodrygo dakika ya 58 akipokea pasi ya mwisho kutoka kwa Vinicius Junior na dakika ya 80 ya mchezo akipokea pasi kutoka kwa Federico Valvede.
Ikumbukwe kuwa katika mchezo wa kwanza, Madrid wakiwa nyumba Santiago Bernabeu wiki iliyopita waliifunga Chelsea bao 2-0, hivyo Madrid ameshinda kwa jumla ya bao 4-0.