Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid waitupa nje Man City Ligi ya Mabingwa Ulaya

IMG 6786.jpeg Wachezaji wa Real Madrid wakishangilia ushindi

Thu, 18 Apr 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Timu ya Real Madrid imefanikiwa kutinga Nusu Fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya kwa penalti 4-3 dhidi ya mabingwa watetezi, Manchester City kufuatia sare ya 1-1 usiku huu Uwanja wa Jijini Etihad Jijini Manchester.

Dakika 120 zilimalizika timu hizo zikiwa zimefungana bao 1-1, mshambuliaji Mbrazil, Rodrigo Silva de Goes akianza kuifungia Real Madrid dakika ya 12, kabla ya kiungo Mbelgiji, Kevin De Bruyne kuisawazishia Manchester City dakika ya 76.

Matokeo hayo yakafanya sare ya jumla 4-4 kufuatia Real Madrid nayo kulazimishwa sare ya 3-3 nyumbani. Baada ya dakika 120, kwenye mikwaju ya penalti waliofunga za Real Madrid ni Jude Bellingham, Lucas Vázquez, José Ignacio Fernández ‘Nacho’ na Antonio Rüdiger, wakati Luka Modrić pekee alikosa.

Waliofunga za Manchester City ni Julián Álvarez, Philip Foden na Ederson Santana de Moraes, huku Bernardo Silva na Mateo Kovačić wakikosa.

Sasa Real Madird itakutana na Bayern Munich ambayo imeitoa Arsenal.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live