Real Madrid imeibuka Bingwa wa Kombe la Vilabu la FIFA (FIFA Club World Cup) na kuweka rekodi ya kushinda ubingwa mara tano baada ya kuinyuka Al Hilal ya Saudi Arabia bao 5-3.
Katika mchezo huo wa fainali uliopigwa jana Jumamosi Februari 11, 2023, mabao ya Madrid yalifungwa na Federico Valverde (18′, 58′) na Vinicius Jr (13′, 69′) na Karim Benzema (54′).
Mchezo huo ambao Madrid walitawala kwa kiasi kikubwa katika Dimba la Prince Moulay Abdallah huko Rabat nchini Morocco, licha ya Waarabu hao wa Saudi Arabia Al Hilal kufanikiwa kufunga bao 3 zilizowekwa kimyani na Luciano Vietto (63′ na 79′) na Moussa Marega aliyefunga dakika ya 26′.
Kabla ya Ubingwa huo, Real Madrid wamewahi kunyanyua kwapa wakishinda ndoo hiyo ya FIFA Club World Cup mwaka 2014, 2016, 2017 na 2018.