Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid kumbeba Haaland kimchongo

Haaland Vs Young Boys Erling Haaland

Mon, 13 Nov 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Real Madrid inadaiwa kuwa kwenye mpango wa kutaka kutumia kipengele kilichopo kwenye mkataba wa straika wa Manchester City, Erling Haaland ambacho kinamuwezesha kuondoka ikiwa timu inayomtaka italipa kiasi cha Euro 200 milioni.

Wakala wa supastaa huyu kwa sasa Rafael Pamenta ambaye alikuwa akifanya kazi kama mwanasheria wa Mino Raiola kwenye masuala ya mpira wa miguu kathibitisha kuwa Haaland ana kipengele cha kumruhusu kuondoka ikiwa atataka kufanya hivyo.

Hata hivyo, haijajulikana moja kwa moja ni kiasi gani kinahitajika ili kuuvunja mkataba wake huo lakini taarifa za ndani kutoka vyanzo vinavyoaminika kwa mujibu wa tovuti ya AS ni kwamba timu ikiwa na Euro 200 milioni inaweza kuipata huduma yake.

Kiasi hicho cha fedha hakionekani kuwa kikubwa sana kwa Real Madrid na kwa sababu hiyo tetesi zinadai huenda akatua kwenye kikosi hicho kama mambo yatakwenda vizri utakapofika wakati wa dirisha kubwa lijalo.

Mkataba wa Haaland unamalizika ifikapo 2027 na msimu huu amefunga mabao 15 kwenye mechi 17 za michuano yote Ulaya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live