Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid Wazidi Kumkomalia Mbappe

Kylian Mbappe 1 1536x864 Mbappe

Sun, 5 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mipango ya Real Madrid ndani na nje ya uwanja ni kuhakikisha inafanikiwa kumnasa mshambuliaja wa Paris Saint-Germain Mfaransa Kylian Mbappe, 22.

Ikiwa zimesalia siku 28 Kylian Mbappé kuingia kwenye miezi sita ya mwisho ya kandarasi yake na Paris Saint-Germain ambapo itaweza kumfanya kuwa huru kuingia saini ya makubaliano ya awali na Real Madrid, hali inayoonekana kuwa ya uhakika zaidi ndani ya Bernabéu.

Madrid wana uhakika wamemchukua mshambuliaji huyo na ushahidi wa imani ya Real kuwa Mbappe atawasili kama mchezaji huru majira ya joto umeanza kuonekana katika mipango ya klabu na kibiashara.

Mbappé anafahamu kuwa kushinda Ballon d’Or ni rahisi zaidi akiwa Real Madrid kuliko alipo sasa PSG.

Alipokuwa na umri wa miaka 18 alishika nafasi ya nne kwenye tuzo hizo wakati ambapo aliiongoza timu yake ya taifa ya Ufaransa kushinda taji la World Cup mwaka 2018.

Baada ya mitatu kupita amerudi nyuma kwa nafasi tano, hiyo inadhihirisha kuwa bado hawezi kutimiza lengo lake la kushinda tuz hiyo akiwa ndani ya PSG na kutamani kutua Real Madrid klabu ambayo role model wake Cristiano Ronaldo amewahi kuitumikia na kutwaa tuzo hiyo.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live