Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid: Tupeni James Tunawapa Hazard

Eden Hazard Reece James 800x420 Madrid yataka mabadilishano

Tue, 28 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid imeamua kufanya dili la kibabe na Chelsea endapo wanataka kumrejesha Eden Hazard katika viunga vya Stamford Bridge katika majira ya usajiri ya kipindi cha baridi.

Real Madrid wako tayari kumtoa Eden Hazard kurudi Chelsea kama sehemu ya makubaliano ya kumnunua Reece James, kulingana na jarida la michezo la El Nacional.

Taarifa ndani ya klabu hiyo zinasema wapo tayari kufanya usajili mpya beki wa kulia kusaidiana na Dani Carvajal, na meneja Carlo Ancelotti amemtaka rais Florentino Perez kumnunua Reece James.

Perez anatarajia kusuluhisha matatizo mawili kwa moja kwa kumleta James na kumrudisha Hazard katika klabu waliyomsajili kama sehemu ya makubaliano sawa.

Ingawa Roman Abramovich angefurahi kumrejesha Hazard London, lakini hataki ije kwa gharama ya mmoja wa wachezaji nyota wa timu yake kuondoka.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live