Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madrid Mabingwa wa La Liga

Madrid Yt(1).jpeg Madrid Mabingwa wa La Liga

Sun, 5 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Real Madrid wametangazwa machampioni wapya wa La Liga baada ya ushindi wa 3-0 walioupata dhidi ya Cadiz huku mahasimu wao wa Barcelona wakipokea kipondo cha 4-2 kutoka kwa Girona na kuzima matumaini ya kutokea maajabu kwenye mbio za ubingwa wa ligi kuu nchini Uhispania

Madrid wametangazwa mabingwa baada ya kufikisha alama 87 kwenye michezo 34 tu alama ambazo haziwezi kufikiwa na timu yoyote wakati huu michezo minne ikiwa imesalia kabla ya kutamatishwa rasmi kwa msimu wa ligi hiyo.

Huu ni ubingwa wa 36 wa La Liga kwa Real Madrid huku likiwa taji la sita la ligi kuu kwa mwalimu Carlo Ancelotti aliyetwaa mataji kwenye ligi zote kubwa Ulaya ambapo kwa Hispania ni mara yake ya pili kubeba taji la ligi kuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live