Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madeni kuzigharimu Porto na Sporting CP

Sportin 696x392 Sporting CP

Sat, 4 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Porto na Sporting CP zinakabiliwa na adhabu ya kufungiwa mwaka mmoja kutocheza Ulaya iwapo zitashindwa kulipa madeni ambayo bado haijalipwa kufikia mwisho wa mwezi ujao.

UEFA siku ya Ijumaa ilifichua vikwazo ambavyo vimetolewa kwa vilabu vinane kwa kukiuka kanuni za Financial Fair Play (FFP).

Vinara wa Ligi ya Premeira Liga Porto na Sporting inayoshika nafasi ya pili wametozwa faini ya Euro laki 300,000 na 250,000 na hawatacheza michuano ya UEFA ya vilabu watakayofuzu katika moja ya misimu mitatu ijayo isipokuwa kama wanaweza kuthibitisha ifikapo Januari 31, 2022 kuwa wamemalizana kulipa “kiasi ambacho kimesalia.”

Klabu ya LaLiga, Real Betis imepigwa faini ya Euro laki 250,000, huku CSKA Sofia na CD Santa Clara zote zikitakiwa kulipa Euro elfu 75,000 na Mons Calpe SC lazima watoe Euro Elfu 15,000.

Vilabu vyote hivyo pia vinakabiliwa na kukosa kucheza Europa League katika msimu wa 2022-23, 2023-24 au 2024-25 kama watafuzu, lakini hawajalipa deni.

FC Astana na CFR 1907 Cluj zilitozwa faini ya Euro laki 150,000 na 200,000, lakini hawakutishiwa kufungiwa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live