Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madega alivyomuwekea Ngumu Ivo Mapunda enzi za uhai wake

Imani Madega .jpeg Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega

Sat, 10 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga, Imani Madega amefariki dunia leo, lakini atakumbukwa kwa misimamo na mbinu alizokuwa anatumia kusajili mastaa ndani ya kikosi hicho.

Madega wakati wa uhai wake amefanya mambo mengi kwenye siasa, soka na uwakili, alisimamia anachokiamini hata kama lingetokea kundi la watu kimpinga hakuyumbishwa.

Katika mahojiano na Mwanaspoti hivi karibuni alisimulia kwamba "Kuna kosa alifanya Ivo Mapunda kipindi hicho alikuwa kipa namba moja na kiwango Cha juu, nikamsimamisha, nikapigiwa simu na kiongozi mmoja mkubwa, nilimgomea, kusema ukweli kwa nafasi ya kiongozi huyo nilipaswa nitekeleze na siyo kugoma ,ila nilifanya vile kuweka unyoofu"

Kwenye mbinu za usajili "Mwaka 2009 nilipewa jukumu la kumsajili Haruna Moshi "Boban' nikaenda kumfuata Uwanja wa Muhimbili ambako alikuwa anafanya mazoezi, Simba ikaniwahi, siku iliyofuata nikawa kituko magazetini vichwa vya Habari viliandika Madega achomeshwa mahindi.

"Baada ya muda kupita nikawalipa kwa kumsajili kipa wao namba moja, Juma Kaseja nilimtumia mdogo wangu Beka, kumshawishi nikaenda kumsainisha hotelini.

Madega baada ya kumaliza uongozi wake Yanga, alihamia Chalinze nyumbani kwake ambako alikuwa ana ofisi ya Uwakili, alikuwa anajishughulisha na kilimo na ufugaji.

Madega amefariki Leo asubuhi na mwili wake unatarajia kupumzishwa kesho mchana, huko huko Chalinze.

Chanzo: Mwanaspoti