Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Madee ampa maua yake Wallace Karia

Madee X Kariaaaaa Madee ampa maua yake Wallace Karia

Mon, 11 Mar 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kutoka Kwenye Ukurasa Wa Instagram wa Msanii wa Bongo Fleva, Madee Ali (Madee) ameandika;

"Kioo kina kawaida ya kuonyesha taswira ambayo ni kioo chenyewe lakini hukigeuza na kuwa ya yule anayekitazama.

Hivyo ni ngumu kuibishia taswira iliyoko kwenye kioo kuwa sio ya Wewe unayekitazama labda maisha ya huko kuzimu ambako maji yanaweza kugeuzwa kuwa damu.

Leo natamani kuileta taswira ya Mpira wa Miguu nchini kupitia Kioo chake ambacho ni Raisi wa TFF Ndugu Wallece Karia.

Hivi kuna Mtanzania asiyeona ukubwa wa picha angavu aliyoichora kwenye mpira wetu toka aliposhika wadhifa wa kuliongoza shirikisho letu la Mpira wa Miguu nchini?basi acha nigusie machache.

1. Mafanikio ya kupanda kwa viwango vya Soka kuanzia Timu za Taifa na Vilabu vyetu, huwezi kuyatenganisha na umadhubuti wa Wallece Karia

2. Mahusiano ya Kimataifa baina ya Shirikisho letu na Taasisi zingine za Kimpira hususan FIFA na CAF.

3. Thamani ya ligi yetu imepanda na kuwa ligi inayovutia kutazamwa na kuvuta kandarasi za Wachezaji wakubwa kwakuwa wanauhakika wa kufikia malengo na maslahi mazuri.

4. Thamani ya Wachezaji wetu imepanda hata katika medani za Kimataifa na wamekuwa tegemeo na tishio, haya huwezi kuyatenga na mikakati ya ndani.

5. Haya mafanikio ya kushiriki AFRICON na Vilabu vyetu kushiriki Mashindano ya CAF kwa mafanikio yanachagizwa na umadhubuti wa Uongozi ambao Karia anasukuma jahazi.

Ni muhimu ifahamike kuwa Wallece Karia amaekua kiunganishi kizuri baina ya Shirikisho letu la Mpira na Serikali, jambo hili limeiwezesha Serikali kupata mawanda mapana ya kutekeleza Sera ya michezo kwa urahisi.

HONGERA SANA WALLECE KARIA, WEWE NI KIOO CHA MATOKEO YA PICHA TUNAYOIONA. @tanfootball"

Chanzo: www.tanzaniaweb.live