Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maddison azidi kuivuruga Spurs

James Maddison To Spurs.jpeg James Maddison

Mon, 26 Jun 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Tottenham itaongeza juhudi za kumsajili James Maddison kutoka Leicester City wiki hii, lakini ofa iliyotolewa na Newcastle United kwaajili ya kungo huyo huenda ikatibua mipango yao.

Kocha mpya wa timu hiyo Ange Postecoglou, anataka kikosi chenye wachezaji wenye ubunifu msimu ujao huku akimpendekeza Maddison.

Taarifa zimeripoti wiki iliyopita kwamba Maddison yuko mbioni kutua Spurs, baada ya Newcastle kukamilisha uhamisho wa Sandro Tonali akitokea AC Milan.

Hata hivyo, licha ya kutumia Pauni 55 mlioni kumnunua mchezaji huyo wa kimataifa wa Italia, mwenye umri wa miaka 21, Newcastle inaamini bado inaweza kuinasa pia saini ya Maddison.

Leicester inataka Pauni 60 milioni ili kumuuza kiungo huyo mwenye umri wa miaka 26, ambaye amebakiza mwaka mmoja kwenye mkataba wake, lakini ofa ya awali la Spurs ni nusu ya kiasi hicho.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live