Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maddison aitwa England

James Maddison Rio Ferdinand F365 James Maddison

Thu, 10 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchezaji wa klabu ya Leicester na timu ya taifa ya England James Maddison amefanikiwa kuitwa kwenye kikosi cha mwisho cha timu ya Taifa ya England kilichotangazwa jioni hii kuelekea kombe la dunia nchini Qatar mwezi huu.

Kumekua na minong’ono ya muda mrefu ambayo imekua ikiendelea kutokana na kocha wa timu ya taifa ya Uingereza kutompa nafasi kiungo huyo wa Leicester kwenye timu yake ambayo amekua akiita.

Kiungo Maddison amekua akionesha ubora mkubwa kwenye klabu yake ya Leicester kwa misimu kadhaa sasa lakini hakua anaitwa kwenye timu ya taifa ya nchi hiyo chini ya mwalimu Gareth Southgate kitu ambacho kimekua kikiibua mijadala sana juu ya kocha huyo.

Lakini leo hii Maddison ameitwa kwenye kikosi cha timu hiyo kitakachoshiriki michuano ya kombe la dunia mwezi huu nchini Qatar na watu wengi wamepongeza jambo hilo na kueleza kua kiungo huyo amestahili kuwepo kwenye kikosi hicho.

Licha ya wadau kupongeza kuitwa kwa kiungo huyo lakini lawama zimeshushwa kwa kocha Southgate baada ya kuwacha wachezaji kama Fikayo Tomori, Tammy Abraham ambao wameonesha ubora mkubwa kwenye vilabu vyao.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live