Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Machinjioni; ukienda viwanja hivi, hutoki salama

Machinjioni Machinjioni; ukienda viwanja hivi, hutoki salama

Thu, 2 Feb 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Msimu wa Ligi Kuu Bara upo mzunguko wa pili na hadi sasa Yanga inaongoza msimamo ikiwa na pointi 56 ikiwazidi watani zao Simba kwa pointi sita walio nazo 50.

Utamu wa ligi hii unakwenda sambamba na upinzani baina ya timu shiriki huku rekodi kadhaa zikiwekwa ikiwamo ya ushindi wa mechi za nyumbani.

Unapafahamu ‘machinjioni’? Hii ni sehemu ambayo wanyama hupelekwa ili wakageuzwe kitoweo na wakipelekwa huko huwa hawatoki salama.

Kwenye Ligi Kuu zipo klabu zimeweka rekodi ya kutofungwa nyumbani na mara nyingi zimekuwa zikipata ushindi - kwa kuwa kila timu inayotua viwanja vyao ni kama imefika machinjioni haitoki salama.

Mwanaspoti linakuletea timu ambazo zimekuwa na rekodi nzuri nyumbani na hata wapinzani wanapotua kwenye viwanja hivyo, wanajua tu kupona sio rahisi.

GEITA GOLD

Baada ya ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Coastal Union Januari 23 mwaka huu mchezo wa Ligi Kuu Bara, Geita Gold imefikisha michezo 35 ya Ligi (Ligi Kuu na Daraja la Kwanza) katika Uwanja wa Nyankumbu bila ya kupoteza.

Takwimu hiyo haihusiani na michezo ile ya Simba na Yanga ambayo imekuwa ikichezwa Uwanja wa CCM Kirumba.

Rekodi hiyo ya ‘Unbeaten’ kwenye Uwanja wa Nyankumbu ilianza msimu wa 2020-2021 wakati timu hiyo ikiwa First Division League (FDL), sasa ikiitwa Championship na ilicheza michezo nane ya nyumbani na kushinda yote bila ya kuruhusu bao huku ikipoteza mitatu na sare moja ugenini.

Katika michezo 16 ya Daraja la Kwanza, Geita ilishinda 12, sare moja na kupoteza mitatu na ilifunga mabao 25 na kuruhusu sita ikivuna pointi 37 ikiwa kileleni na kupanda rasmi Ligi Kuu Bara.

Msimu wake wa kwanza Ligi Kuu (2021-2022), ilimaliza katika nafasi ya nne na kukata tiketi ya kushiriki Kombe la Shirikisho Barani Afrika huku ikifika robo fainali ya Kombe la Azam (ASFC).

Michezo 15 ya nyumbani ilicheza 13 Uwanja wa Nyankumbu ikishinda nane na sare tano huku miwili ya Simba, Yanga ikichezwa CCM Kirumba.

Msimu huu wa 2022/23, michezo iliyoshinda Nyankumbu ni 2-1 na Namungo FC, (1-0) v Ihefu, (2-0) v Dodoma Jiji, (1-0) v Coastal Union huku sare ni (1-1) v KMC, (2-2) v Mtibwa Sugar, (1-1) v Azam FC na (1-1) v Polisi Tanzania.

Mechi tatu zilizopigwa CCM Kirumba ilipoteza 1-0 dhidi ya Yanga, 1-1 na Singida Big Stars kisha 5-0 na Simba.

SIMBA

Simba ina rekodi nzuri inapocheza uwanja wa nyumbani kwani tangu mara ya mwisho ilipofungwa na Yanga bao 1-0, Julai 3, 2021, imecheza michezo 27 mfululizo bila ya kupoteza ikishinda 24 kisha sare mitatu, kumbuka walifungwa na Azam lakini Azam ndiye aliyekuwa nyumbani.

Michezo iliyoshinda ni (4-1) v Mbeya City, (4-0) v Namungo, (2-0) v Coastal Union, (1-0) v Polisi Tanzania, (1-0) v Namungo FC, (2-1) v Geita Gold, (2-1) v Azam FC na (1-0) v Tanzania Prisons.

Ushindi mwingine ni (1-0) v Mbeya Kwanza, (3-0) v Biashara United, (2-0) v Dodoma Jiji, (4-1) v Ruvu Shooting, (2-0) v Kagera Sugar, (3-0) v Mbeya City, (3-1) v KMC na (2-0) v Mtibwa Sugar.

(3-0) v Geita Gold, (2-0) v Kagera Sugar, (3-0) v Dodoma Jiji, (5-0) v Mtibwa Sugar, (1-0) v Ihefu, (1-0) v Namungo FC, kichapo kizito cha (7-1) v Tanzania Prisons na (3-2) v Mbeya City.

Michezo mitatu ya suluhu ni (0-0) v Coastal Union, (0-0) v Yanga na sare ya kufungana mabao 2-2 na KMC.

Katika michezo hiyo safu ya ushambuliaji ya Simba imeonekana tishio kwa wapinzani wake kwani imefunga jumla ya mabao 64 huku kwa upande wao wakiruhusu nyavu zao kutikiswa mara 10 tu.

YANGA

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Bara, Yanga ina rekodi yao pia ya kipekee kwani tangu mara ya mwisho ilipofungwa bao 1-0 na Azam Aprili 25, 2021 ilicheza jumla ya michezo 49 bila kupoteza.

Rekodi hiyo ilidumu hadi Novemba 29 mwaka jana wakati kikosi hicho kilipofungwa mabao 2-1 dhidi ya Ihefu, Uwanja wa Highland Estate na kuwashangaza mashabiki wengi nchini kutokana na kiwango chao bora.

Mchezo na Azam FC ulikuwa pia wa mwisho kupoteza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa kwani baada ya hapo imecheza jumla ya mechi 29 na kati ya hizo imeshinda 24 huku mitano ikiisha kwa sare.

Michezo ya ushindi ni (3-1) v Gwambina, (3-2) v Mwadui, (2-0) v Ihefu, (1-0) v Geita Gold, (2-0) v Azam FC, (3-1) v Ruvu Shooting, (2-1) v Biashara United, (4-0) v Dodoma Jiji, (3-0) v Kagera Sugar.

(2-0) v KMC, (2-1) v Namungo FC, (4-0) v Mbeya Kwanza, (3-0) v Coastal Union, (2-0) v Polisi Tanzania, (1-0) v Mtibwa Sugar, (3-0) v Mtibwa Sugar, (1-0) v KMC, (4-1) v Singida Big Stars. (2-0) v Mbeya City, (1-0) v Tanzania Prisons, (3-0) v Polisi Tanzania, (3-0) v Coastal Union, (1-0) v Ihefu na (1-0) v Ruvu Shooting. Michezo ya sare ni (0-0) v Mbeya City, (0-0) v Simba, (0-0) v Tanzania Prisons, (2-2) v Azam FC na (1-1) v Simba. Katika michezo hiyo eneo la ushambuliaji la Yanga limefunga mabao 59 na kuruhusu 10.

AZAM FC

Ukiachana na kichapo cha mabao 3-2 ilichokipata Azam kutoka kwa Yanga kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa Desemba 25, mwaka jana ila miamba hii ina rekodi nzuri inapocheza katika Uwanja wa Azam Complex.

Mara ya mwisho kupoteza nyumbani ilikuwa kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Polisi Tanzania Machi 5, mwaka jana ila baada ya hapo imecheza jumla ya michezo 15 ikishinda 13 huku miwili ikiisha kwa sare.

Michezo ya ushindi ni (2-1) v KMC, (2-0) v Mbeya Kwanza, (1-0) v Tanzania Prisons, (4-1) v Biashara United, (2-1) v Kagera Sugar, (1-0) v Singida Big Stars, (1-0) v Simba) na (1-0) v Ihefu.

(2-1) v Dodoma Jiji, (1-0) v Ruvu Shooting, (3-2) v Coastal Union, (6-1) v Mbeya City, (3-0) v Tanzania Prisons wakati ile iliyomalizika kwa sare ni (1-1) v Simba na (1-1) v Geita Gold. Safu yake ya ushambuliaji imefunga mabao 31 huku ikiruhusu nyavu zake kutikiswa mara tisa.

MSIKIE PASTORY

Kaimu Katibu Mkuu wa Geita Gold, Liberatus Pastory anasema ni jambo la kujivunia kwa timu yao kuweka rekodi ya kutopoteza katika uwanja wao licha ya kushiriki Ligi Kuu kwa msimu wa tatu.

“Sisi bado ni wageni kwa sababu hatuna muda mrefu ila malengo tuliyojiwekea ni kila mpinzani wetu anayefika hapa Nyankumbu haondoki na pointi kirahisi na ndio maana tumefika hapa tulipo,” anasema.

Chanzo: Mwanaspoti