ALexis Mac Allister amefichua siri kwamba amegoma kuvaa jezi namba 8 Liverpool kwa sababu ina historia kubwa na iliwahi kuvaliwa na mkongwe Steven Gerrard.
Kiungo huyo alisajiliwa na Liverpool kwa Pauni 35 milioni akitokea Brighton mwezi uliopita baada ya kufuatiliwa msimu mzima na kocha Jurgen Klopp.
Baada ya kugoma Mac Allister alipewa jezi namba 10 ambayo atavaa msimu ujao, lakini akaeleza kwanini hakukubali kuvaa jezi namba 8.
"Siku moja nilikuwa nikiongea na Baba yangu mzazi akaniuliza namba gani ningependa kuvaa Liverpool, nilijua kulikuwa namba nyingi ikiwemo namba 8 ambayo ni muhimu sana.
Lakini nikasita kwanza, mwisho nikachagua namba 10, namba 8 ina historia kubwa ya klabu" Pia Mac Allister amesisitiza namba 10 itakuwa na presha kubwa kwa sababu iliwahi kuvaliwa na Sadio Mane na Michael Owen.