Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mac Allister afichua kilichompeleka Liverpool

Jurgen Klopp And Alexis Mac Allister Mac Allister afichua kilichompeleka Liverpool

Thu, 15 Jun 2023 Chanzo: Dar24

Kiungo mpya wa Liverpool, Alexis Mac Allister amefichua namna alivyokubali haraka kwenda kujiunga na miamba hiyo ya Anfield katika dirisha hili la uhamisho wa majira ya kiangazi.

Liverpool imefanikiwa kunasa saini ya Kiungo huyo kutoka nchini Argentina na mshindi wa Kombe la Dunia akitokea Brighton.

Wakati Mac Allister akiwa staa mwenye heshima kubwa Brighton na namna walivyomleta kwenye Ligi Kuu England, amekiri kwamba Jurgen Klopp ndiye aliyemshawishi kutua Anfield, kwa sababu ilikuwa ngumu kumgomea.

“Nilipata nafasi ya kuzungumza naye na ndiye aliyekuwa moja ya sababu ya kufanya uamuzi wangu wa haraka kujiunga na Liverpool,” amesema Mac lister.

“Niliona dhamira yake kutaka kunisajili na hilo lilikuwa muhimu sana. Tulizungumza kuhusu soka, namna anavyoona mambo na dhamira ya klabu katika kubeba mataji.

“Kwenda kujiunga na moja ya klabu kubwa duniani na England ni furaha kubwa na ndoto kubwa. Nataka kuitumia nafasi hii kwa sababu imekuja katika wakati mzuri.

Chanzo: Dar24