Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabululu ruksa kuwavaa Simba CAFCC

Mabululu Mabululu ruksa kuwavaa Simba CAFCC

Wed, 28 Aug 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Klabu ya Al-Ahli Tripoli imethibitisha kuwa wamepata kibali kutoka CAF cha kumtumia mshambuliaji wao mpya Agostinho Cristóvão Paciência maarufu kama Mabululu.

Mabululu alisajiliwa katika dirisha hili kubwa lililopita akitokea Al-Ittihad ya Misri hakucheza mechi yoyote kwa sababu hakuwa na vibali, wameruhusiwa kumtumia kuanzia mechi zijazo za CAF.

Takwimu zake za ligi kuu ya Egypt akiwa Al-Ittihad katika misimu 3!

Season: 23/24

Magoli 11 (mfungaji wa sita)

Assist 5

Season: 22/23

Magoli 16

Asist 1

Season: 21/22

Magoli 13

Assist 2

Wanasimba huyu ndio Mchezaji wa kuchungwa zaidi kwenye mechi mbili dhidi ya Simba SC (home na away).

Al Ahli Tripoli wamekamilisha usajili wa wachezaji wapya saba kwenye usajili wao wa CAF ambao hawakuwa wamesajiliwa katika usajili wa awali ambapo timu hiyo ilicheza dhidi ya Uhamiaji ya Zanzibar na kufuzu kwa goli 5-1 kwenye hatua za awali za CAFCC.

Wachezaji wapya walioingia katika usajili wa CAF ambao watakuwa na uhalali wa kuikabili Simba ni hawa wafuatao:

Hamdou Elhouni

Muaid Ellafi

Sanad Al Warfalli

Ghaylen Chaalali

Al-Gozoli Nooh

Bakhit Khamis

Cristovao Mabululu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live