Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabosi wa Bayern wabakisha siku chache kumshusha Mane

Mane Pic Data Winga wa Liverpool, Sadio Mane

Tue, 31 May 2022 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Bayern Munich ipo kwenye hatua za mwisho kukamilisha dili la staa wa Liverpool na Senegal, Sadio Mane, 30, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi. Imeripotiwa kuwa dili hilo huenda likakamilika kwa kiasi kisichopungua Pauni 34 milioni.

Mkataba wa sasa wa Mane unamalizika mwaka 2023. Msimu huu amecheza mechi 51 za michuano yote na kufunga mabao 23.

Inadaiwa kuwa Mane alikuwa tayari kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye viunga vya Merseyside lakini tatizo lilikuwa kwenye mshahara aliokuwa anauhitaji ambao mabosi wa Liver wameona kwamba hawawezi kumpa.

Munich inaamini Mane ataenda kuwa msaada kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo huenda ikapata pigo katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi kwa kuondokewa na straika wao Robert Lewandowski, ambaye anahusishwa na Barcelona.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz