Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabosi KMC waahidi neema kwa mastaa

Azam FC, Young Africans Zaivuruga KMC FC KMC

Wed, 22 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baada ya muenendo mbaya wa timu ya KMC katika ligi kuu, mabosi wa timu hiyo juzi Jumamosi walikaa chini na wachezaji wao kisha wakafanya kikao kizito kuhakikisha wanaipambania timu hiyo ili ibaki kwenye ligi.

KMC inashika nafasi ya 12 ikiwa na pointi 23, huku ikicheza mechi 22, ikifungwa mechi tisa, sare nane na kushinda tano.

Habari ambazo tumepenyezewa ni kwamba kwenye kikao hicho viongozi waliwataka wachezaji wao wapambane kwenye mechi zilizobaki na watawaongezea bonasi za mechi ambazo walikuwa wanapata awali.

Inadaiwa awali bonasi ya kila mchezo ilikuwa ni sh3 milioni kwa wachezaji wote kwa mechi za mashindano lakini safari hii kwenye kikosi hicho mabosi wamewaambia watatoa donge nono zaidi.

"Kilikuwa ni kikao cha kufahamu tu shida nini na wao kutoa moyo, ni kikao cha ndani ya timu lakini kikiwa ni sehemu ya kuhakikisha tunafanya vizuri,"kilisema chanzo ndani ya Mabosi wa timu hiyo.

Alipotafutwa katibu mkuu wa KMC, Daniel Mwakasungura alisema kwa kifupi;"Kikao cha kawaida ambacho kipo kwenye utaratibu wa klabu na kila baada ya muda tunakaa, kikao cha ndani hakuna stori."

Alipotafutwa msemaji wa timu hiyo, Christina Mwagala alijibu kwa kifupi;"Kikao kilikuwa ni cha ndani hakihusiani na stori."

Kikao hicho kilikuwa na Mkurugenzi wa Manispaa ya Kinondoni Mh Hanifa Suleiman Hamza, Naibu mstahiki Meya wa manispaa ya kinondoni Mh, Josephat Rwegasira, Mwenyekiti wa KMC, Kheri Misinga  na katib mkuu wa timu Daniel Mwakasungura.

Kmc inajiandaa na mchezo dhidi ya Yanga utakaochezwa leo saa 10:00 jioni katika uwanja wa Mkapa.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live