Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabosi Chelsea kushusha Pauni 60 milioni kwa Olise

Michael Olise Chelsea.jpeg Winga wa Crystal Palace na Ufaransa, Michael Olise

Mon, 27 May 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Chelsea inatarajia kutuma ofa ya Pauni 60 milioni kwa ajili ya kumsajili winga wa Crystal Palace, Michael Olise, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi.

Mabosi wa Chelsea wanataka kumsajili nyota huyo ikiwa ni sehemu wa ramani ya timu yao bila kujali ni kocha gani ataajiriwa.

Chelsea imekuwa ikisajili wachezaji wengi vijana ikiamini watakuwa tegemeo kwa muda mrefu na Olise inamuona kama mmoja wa mastaa wanaofaa katika mpango huo.

Matajiri hao wa London watatakiwa kuzipiku Manchester United na Man City ambazo zinahusishwa na huduma yake kwa muda.

Staa huyu wa kimataifa wa Ufaransa mwenye umri wa miaka 22, mkataba wake unamalizika mwaka 2027 na msimu huu amecheza mechi 19 za Ligi Kuu England na kufunga mabao 10.

BORUSSIA Dortmund itafanya mazungumzo na Manchester United kwa ajili ya kumsainisha mkataba wa kudumu winga Jadon Sancho katika dirisha lijalo, lakini inaonekana huenda kukawa na ugumu kwa sababu Man United inahitaji kiasi kikubwa cha pesa. Sancho aliyetua Dortmund kwa mkopo wa nusu msimu majira ya baridi, msimu huu amecheza mechi 23 za michuano yote na kufunga mabao matatu.

AC Milan na Juventus zinatajwa kuwa katika mpango wa kumsajili beki wa Borussia Dortmund na Ujerumani, Mats Hummels, 35, katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo atakuwa huru baada ya mkataba wake kumalizika. Hummels pia anawindwa na timu za Marekani na Saudi Arabia. Msimu huu amecheza mechi 39 za michuano yote na kufunga mabao manne.

WAWAKILISHI wa Arsenal wameanza mazungumzo kwa ajili ya kumsajili kipa wa Feyenoord na Uholanzi, Justin Bijlow, 26, ili awe mbadala wa Aaron Ramsdale anayetarajiwa kuondoka mwisho wa msimu huu. Justin anasajiliwa ili akamsadie David Raya ambaye msimu uliomalizika ndio alikuwa akitumiwa zaidi na Mikel Arteta.

LIVERPOOL inatarajiwa kuingia katika mazungumzo na Benfica wakati wa dirisha lijalo kwa ajili ya kumsajili kiungo wa Benfica, Orkun Kokcu ambaye amependekezwa na kocha mpya Arne Slot anayemtaka kwa ajili ya kuboresha eneo la ulinzi. Orkun ambaye pia anaichezea timu ya taifa ya Uturuki, msimnu huu amecheza mechi 43 za michuano yote.

KIUNGO wa Real Madrid na Croatia, Luka Modric, 38, huenda akaongeza mkataba mpya wa mwaka mmoja utakaomwezesha kusalia katika timu hiyo kwa muda mrefu zaidi. Modric aliyekuwa anahusishwa na timu za Saudi Arabia tangu dirisha lililopita la majira ya baridi, mkataba wake wa sasa unamalizika mwisho wa msimu huu na inadaiwa kwamba ana ofa ya kubaki.

Chanzo: Mwanaspoti