Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabosi Bayern wapambana kuibania Madrid kwa Alphonso Davies

Alphonso Davies Alphonso Davies

Fri, 7 Jun 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Bayern Munich inamshawishi beki wao wa pembeni, Alphonso Davies akubali kusaini mkataba mpya wa kuendelea kusalia kwenye timu yao licha ya Real Madrid kuonyesha nia ya kutaka kumsajili.

Awali ilielezwa Davies angeondoka mwisho wa msimu huu kujiunga na Madrid kisha Bayern ingemsajili beki wa Arsenal Oleksandr Zinchenko kuziba pengo lake.

Kwa sasa mpango huo umekufa na Bayern inataka kumshawishi Davies asaini mkataba mpya wakati ule wa sasa ukienda kumalizika mwisho wa msimu ujao.

Mabosi wa Bayern wamepata nguvu ya kufanya naye mazungumzo ya kumsainisha mkataba mpya baada ya Madrid kuripotiwa kutaka kusubiri hadi mwisho wa msimu ujao atakapokuwa mchezaji huru.

Davies ni mmoja kati ya mastaa walioonyesha kiwango bora kwa muda mrefu katika kikosi cha Bayern na msimu uliomalizika alicheza mechi 42 za michuano yote, amefunga mabao matatu na kutoa asisti sita.

Bayern inataka kuimarisha kikosi chake baada ya msimu uliopita kupoteza taji la ubingwa.

ATLETICO Madrid inajaribu kuwatumia mastaa wao, Angel Correa, Rodrigo de Paul na Nahuel Molina wajaribu kumshawishi straika wa Manchester City, Julian Alvarez akubali kujiunga na timu hiyo dirisha lijalo. Alvarez mwenye umri wa miaka 24, huduma yake pia inahitajika na PÂȘris St-Germain na anaonekana kuhitaji kuondoka ili kutua timu itakayompa nafasi kubwa zaidi ya kucheza kwenye kikosi cha kwanza.

MANCHESTER United imeungana na Liverpool kwenye harakati za kuiwania saini ya beki wa kati wa Lille na Ufaransa, Leny Yoro, 18, katika dirisha hili. Liverpool na Man United zimevutiwa sana na staa huyu kwa sababu umri wake bado ni mdogo, hivyo zinaamini zitamtumia kwa muda mrefu. Timu hizi pia zinataka huduma ya Leny kutokana na upungufu uliopo kwenye safu zao za ulinzi.

Tottenham imepanga kutoa Pauni 50 milioni kwa ajili ya kuipiku Aston Villa kwenye vita ya kuiwania saini ya kiungo wa Chelsea Conor Gallagher katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi ambapo pia anawindwa na Atletico Madrid. Mabosi wa Chelsea wanataka kumuuza staa huyu katika dirisha hili ikiwa ni katika harakati za kukusanya pesa kwa ajili ya kufanya usajili katika dirisha hili.

MABOSI wa Galatasaray wanataka kumsajili mshambuliaji wa Manchester United, Anthony Martial katika dirisha lijalo la majira ya kiangazi lakini amepewa sharti la kukubali kupunguza mshahara wake anaoupokea Man United. Martial haonekani kuwa kwenye mipango ya Kocha Erik ten Hag kwa msimu ujao. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwakani.

KIUNGO wa Fulham Andreas Pereira ambaye anawindwa na Tottenham amesisitiza kwamba ataamua hatma yake baada ya michuano ya Andreas Copa America mwaka huu na atakutana na wakala wake kujadili hilo. Pereira alionyesha kiwango bora kwenye msimu uliomalizika kiasi cha kuivutia Spurs. Mkataba wake wa sasa unatarajiwa kumalizika mwaka 2026.

Newcastle ipo kwenye vita kali dhidi ya Atletico Madrid na Roma kwa ajili ya kuipata huduma ya beki kisiki wa AFC Bournemouth Lloyd dirisha hili. Timu nyingi zimevutiwa na kutaka kumsajili staa huyu kwa sababu ya ubora wake na mkataba wake unaomalizika mwisho wa mwezi huu. Hadi sasa hakuna timu iliyofikia makubaliano ya moja kwa moja na beki huyu.

LIVERPOOL ipo kwenye mchakato wa kutafuta kipa mwingine baada ya kuamua kumruhusu kipa wao, Caoimhin Kelleher, 25, kuondoka dirisha hili. Liverpool inataka kumruhusu Kelleher aondoke kwa sababu Kocha Arne Slot hana mpango wa kumfanya kuwa namba moja na staa huyo anataka kupata namba ya kudumu katika kikosi cha kwanza.

Chanzo: Mwanaspoti