Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabomu ya machozi yatawala mazoezi ya Simba

Mabomu Pic Data Mabomu ya machozi yatawala mazoezi ya Simba

Thu, 18 Nov 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

Jeshi la Polisi limelazimika kutumia mabomu ya machozi kutawanya umati wa mashabiki waliokuwa nje ya uwanja wa CCM Kirumba Mwanza kushuhudia mazoezi ya timu ya Simba.

Hatua hiyo imekuja baada ya mashabiki kugoma kuondoka wakishinikiza kuingia ndani kushuhudia mazoezi hayo.

Jeshi hilo limepiga mabomu matano hewani na kutawanya watu wakikimbia ovyo.

Timu ya Simba inaendelea na mazoezi uwanjani hapo kujiandaa na mchezo wa kesho dhidi ya Ruvu Shooting, huku Waandishi wa habari nao wakiwa hawajaruhusiwa kuingia ndani hadi sasa.

Awali Mratibu wa Simba Abbas Ally alisema waandishi wa habari hawaruhusiwi kuingia kwani kinachohitajika wameshakipata kwenye mkutano wa maandalizi ya mechi uliofanyika mchana.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz