"They bounce back" ingekuwa Ulaya lugha hiyo ingekuwa Yanga ipo huko ingetumika lugha ya aina hiyo baada ya kupata ushindi dhidi ya Geita uliotokana na wao kupoteza mechi iliopita dhidi ya Ihefu FC.
Hemed Morocco na vijana wake walifikiria zaidi hasira za Yanga kuliko uhalisia wa mechi yenyewe uliopelekea mwalimu kwenda na mid block na plan B yake ikawa kushambulia kwa kustukiza/ counter Attack kwa bahati mbaya baada ya kuumia Elias Maguli kila kitu kiliishia pale.
Ni kama tu Yanga walifikiria zaidi idadi ya mabao kwendana na muda uliopo baada ya Geita kuamua kuwa nyuma na kusubiri maajabu ya mpira yatokee ikawa ni kuonyeshwa mbinu za Gamond kule Avic town huwa wanafundishwa nini wakina Aucho,Muda na Pacome pindi unapokutana na timu inayoamua kucheza nyuma ya mpira.
Baada ya mabao mawili ya haraka ya Pacome na Aziz Ki kwa hali ya kawaida ilikuwa nguma Geita kuendelea kuwa nyuma.
Bao la Max Nzengeli lilimaliza kila kitu lakini jumla ya mabao yote bado yanaipa Yanga homework ngumu ya eneo la mshambuliaji wa mwisho kutokana na kushindwa kuwa na mfungaji katika eneo hilo kwa muda mrefu bado Clement Mzize na Musonda wakiungana na Konkoni wana struggle kwa kiasi kikubwa.