Criatiano Ronaldo anachukuliwa kuwa mmoja wa wachezaji bora katika zama za kisasa.
Rekodi ya Ronaldo inajieleza yenyewe jinsi nyota huyo wa Ureno alivyo mmoja wa wachezaji bora zaidi kuwahi kutokea duniani.
Ronaldo pia amebadilisha mchezo wake sana ili kukabiliana na umri. Alianza uchezaji wake kama winga mwenye kasi ambaye angeweza kufanya fujo dhidi ya safu ya ulinzi, lakini sasa anaangazia kuuweka mpira wavuni kwa ufanisi mkubwa.
Bado anaweza kuwapita wachezaji, lakini si kwa masafa aliyozoea. Mabeki bado wanatakiwa kufanya kazi kwa bidii ili kubana harakati zake na kumzuia asifunge bao.
Kwa maelezo hayo, hawa hapa ni mabeki watano ambao wamefanikiwa kujilinda dhidi ya supastaa huyo wa zamani wa Manchester United kwa miaka mingi...
#5. Sergio Ramos
Moja ya faida za kuwa wachezaji wenzake na Ronaldo ni kwamba unajifunza jinsi anavyocheza. Sergio Ramos na Alvaro Arbeloa walitumia faida hiyo dhidi yake wakati Ureno ilipokutana na Hispania kwenye Euro 2012.
Ureno walikuwa wamebakisha hatua mbili pekee kufikia ndoto yao kulibeba kombe hilo walipokutana na Hispania katika hatua ya nusu fainali ya mashindano hayo.
Hakukuwa na mikwaju yoyote iliyolenga lango kwani pande zote mbili zilichagua kucheza kwa kujilinda iwezekanavyo, lengo likiwa ni kutoruhusu kufungwa.
Ronaldo ni mchezaji mmoja anayeweza kuvunja msukosuko hata kama timu haichezi katika ubora wake. Lakini katika hafla hii, hakuweza kushawishi mchezo licha ya juhudi zake bora.
Hii kwa kiasi kikubwa ilitokana na jinsi Ramos na Arbeloa walivyoweza kumzuia. Hawakumpa nyota huyo wa Ureno mapumziko ya dakika moja na walimfanya anyamaze kwa muda wote.
#4. Eric Abidal
Eric Abidal alikuwa na kazi nzuri sana akiwa na Barcelona. Alikuwa sehemu ya kikosi maarufu cha Pep Guardiola ambacho kilishinda kila kitu katika njia yao. Moja ya usiku wake wa kukumbukwa ulikuja wakati yeye na timu ya Barcelona walipoirarua Real Madrid.
Ilikuwa ni mara ya kwanza kukutana kati ya Jose Mourinho na Pep Guardiola kwenye La Liga. Real Madrid walisafiri hadi Camp Nou wakitaka kupunguza uongozi wa Wakatalunya hao.
Haikuwa mara ya kwanza kwa Ronaldo kukutana na Wakatalunya, lakini alinyamazishwa sana na walinzi. Barcelona walitawala sehemu kubwa ya umiliki wa mpira.
Mpinzani wa Ronaldo, Lionel Messi alikuwa na mchezo wa ajabu, wakati nyota huyo wa Ureno hakupewa nafasi au muda wa kufanya mashambulizi ya aina yoyote - shukrani kwa Abidal.
Mfaransa huyo alijua jinsi Ronaldo anavyoweza kuwa hatari kwenye winga. Hii ndiyo sababu alijitahidi sana kuhakikisha kwamba Ronaldo hapiti.
Usiku huo, safu ya nyuma ya nne iliwaweka kimya sana washambuliaji wa Real Madrid. Ulikuwa ni usiku ambao Ronaldo angetaka kuusahau. 'Los Blancos' walikumbana na kipigo cha mabao 5-0 kwenye mechi ya El Clasico, huku Abidal akijiweka sawa dhidi ya mmoja wa wachezaji bora katika soka duniani.
#3. Alessandro Nesta
Alessandro Nesta ni mmoja wa wachezaji waliopambwa zaidi na AC Milan kama beki mkubwa. Pamoja na Paolo Maldini, aliunda ushirikiano karibu usioweza kupenyeka nchini Italia.
Sir Alex Ferguson hakuwa na kawaida ya kupoteza mara nyingi sana, lakini dhidi ya Milan, timu yake ya Manchester United ilitolewa kabisa. Licha ya kujivunia Wachezaji kama Wayne Rooney, Cristiano Ronaldo na Ryan Giggs katika safu ya ushambuliaji, United hawakuwahi kuitisha timu ya AC Milan.
Nesta, siku hiyo, hakuwa na Maldini kando yake, lakini mabeki wengine walimpa sapoti ya kutosha kuisimamia safu ya ulinzi. Rooney na Ronaldo walizoea kubadilishana nafasi, lakini hakuna hata moja kati ya hizo iliyofanya kazi dhidi ya safu ya nyuma ya Milan.
Manchester United ilipeperushwa na timu ya Milan katika kipindi cha kwanza huku Clarence Seedorf akifunga mara mbili na kuwafanya wasonge mbele kwa mabao 2-0. United walimiliki mpira zaidi kipindi cha pili, lakini Ronaldo hakuweza hata kupiga shuti la maana lililolenga lango.
Milan walikuwa wameundwa kwa kiwango cha juu katika ulinzi na yote yalitokana na usomaji wa Nesta wa mchezo na ushirikiano na washirika wake wa ulinzi.
#2. Ashley Cole
Ashley Cole na Ronaldo walikutana mara kadhaa kwenye Ligi Kuu England.
Wakati Cole alipokuwa Arsenal, Ronaldo alikuwa kijana ambaye alicheza bila hofu. Ronaldo alikuwa bidhaa isiyojulikana wakati huo, ambayo ilifanya iwe vigumu kwa mabeki kumtabiri.
Hata hivyo, Cole alimrudisha wakati akiwa na Chelsea na hata wakati England ilipokutana na Ureno. Alijifunza jinsi ya kubadilisha hila za Ronaldo kwa kushikamana naye karibu iwezekanavyo na kimsingi kumtoa nje ya mchezo.
Ronaldo amewahi kusema kwamba, Cole ni mmoja kati ya wapinzani wagumu aliowahi kukutana nao.
"Kwa miaka mingi nilikuwa na vita kubwa na Ashley Cole, hakupi sekunde ya kupumua. Alikuwa mchezaji shupavu sana alipokuwa kwenye kilele chake, mwepesi, mgumu katika kukaba."
#1. Diego Godin
Atletico Madrid, chini ya Diego Simeone, imekuwa na nguvu ya kutegemewa, ndani na pia Ulaya. 'Rojiblancos' hao wanajivunia rekodi nzuri sana dhidi ya wapinzani wao wa jiji chini ya El Cholo.
Mchezaji mmoja, haswa, amepata sifa kubwa kutoka kwa wachambuzi kote ulimwenguni kwa ubora wake katika safu ya ulinzi. Diego Godin, enzi zake katika mji mkuu wa Hispania, alikuwa mwamba wa Atletico Madrid, kwani aliisaidia timu hiyo kupata sifa ya kuwa moja ya timu ngumu zaidi kuifunga Ulaya
Real Madrid waligundua mara kadhaa dhidi ya majirani zao jinsi ilivyo ngumu kuwashinda. Kando na fainali za Ligi ya Mabingwa Ulaya 'Los Blancos', katika misimu ya hivi karibuni, hawajapenda kucheza Atletico.
Moja ya mechi mbaya zaidi ya Ronaldo ilikuja dhidi ya Atletico mnamo mwaka 2015 walipochapwa mabao 4-0 ugenini. Ronaldo alipata mshtuko, baada ya kutolewa nje ya mchezo na walinzi wa Atletico.
Los Blancos walikuwa na mashuti manne pekee yaliyolenga lango, huku moja pekee likilenga lango. Ronaldo alilipiza kisasi msimu uliofuata kwa kufunga hat-trick dhidi ya Atletico.