Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabeki, viungo na vita ya asisti

Yanga Mastaa , Pacome, Yao Mabeki, viungo na vita ya asisti

Tue, 31 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

LIGI Kuu Bara, sasa ipo mzunguko wa nane huku ikiwa na burudani ya aina yake moja wapo ni vita ya kutoa pasi za mwisho 'asisti', iliyopo kati ya mabeki na viungo.

Miaka ya nyuma ilikuwa ngumu kumuona beki akiongoza kwenye orodha ya asisti ila kwa sasa mabeki hauwaambii kitu kwenye kuasisiti kwani nao wameingia kwenye mfumo huku wakiongoza kwenye 10 bora ya waliotoa Asisti nyingi hadi sasa lakini pia wakiwa karibu nusu ya wachezaji wenye asisti mbili hadi sasa.

Beki wa Yanga, Kouassi Attohoula ndiye anaongoza orodha ya kutoa asisti akiwa nazo nne lakini anafuatiwa na mabeki wengine, David Bryson wa JKT Tanzania, Shomari Kapombe na Mohamed Hussein wa Simba na Lusajo Mwaikenda wa Azam ambao kila mmoja anazo mbili.

Kwa viungo, ukiwatoa Luis wa Simba na Ladack Chasimbi wa Mtibwa wenye nazo tatu wengine ni Kibu Denis wa Simba, Maxi Nzengeli wa Yanga, Impiri Mbombo wa Tabora United, Jacob Masawe wa Namungo na Awesu Awesu wa KMC wenye mbili kila mmoja.

Wachezaji wengine wengi wana asisiti moja moja. Hata hivyo namba hizi ni kabal ya mechi tatu za jana ambapo JKT iliikaribisha Dodoma Jiji, Tanzania Prisons ikawa mwenyeji wa Geita Gold na Kagera Sugar ikawa ukawaalika Tabora United.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: