Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabeki hawa wamelibeba Taifa - Mchambuzi

Nondo Job Bacca Mabeki hawa wamelibeba Taifa - Mchambuzi

Sat, 9 Sep 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mchambuzi wa Tv3, Boiboi Mkali amesema kuwa, ubora wa safu ya ulinzi ya Timu ya Taifa ya Tanzania ndiyo umesababisha kwa asilimia kubwa Taifa Stars kufuzu michuano ya fainali ya AFCON 2023 juzi dhidi ya Algeria.

Tanzania imefanikiwa kufuzu fainali za AFCON 2023 usiku wa juzi baada ya kitoa sare ya bila kufungana na Timu ya Taifa ya Algeria katika Dimba la May 19, nchini humo.

Matokeo hayo yalizifanya Algeria kufikisha alama 16 akiwa kinara wa kundi na Tanzania alama 8 katika nafasi ya pili, alama hizi hazingeweza kufikiwa na timu yoyote kwenye kundi hilo, hivyo Uganda na Niger wakaaga mashindano dakika za lala salama.

"Ubora wa safu ya ulinzi katika kikosi cha Timu ya Taifa Stars katika mchezo dhidi ya Algeria ndiyo umepelekea kwa nafasi kubwa kufuzu fainali zijazo za Afcon nchini Ivory Coast

"Mabeki watatu wa kati kwenye eneo la kujilinda, Ibrahim Bacca, Dickson Job na Bakari Mwanyeto walikuwa katika kiwango bora sana dhidi ya washambuliaji wa Algeri.

"Hii pia inatokana na ubora uliotengenezwa kwenye kikosi chao cha Yanga chini ya kocha Nabi," ameandika Mchambuzi wa TV3, Boiboi Mkali.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live