Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabeki Ihefu wamzingua Maxime

Ihefu Mabekiiiii Mabeki Ihefu wamzingua maxime

Thu, 15 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Licha ya kuchekelea matokeo ya ushindi, Kocha mkuu wa Ihefu, Mecky Maxime amesema bado hajafurahishwa na kiwango cha mabeki wake kutokana na kuruhusu idadi kubwa ya mabao akiwafungia kazi Geita Gold.

Maxime akiiongoza timu hiyo kwa mara ya kwanza alianza kwa kishindo akiwalaza Mtibwa Sugar mabao 3-2 na sasa wanajipanga upya na mchezo ujao dhidi ya Geita Gold Februari 19, mkoani Geita, mchezo wa mzunguko wa pili Ligi Kuu.

Matokeo hayo yaliifanya Ihefu kupanda nafasi ya 11 kwa pointi 16, huku Geita Gold waliopoteza mchezo wao dhidi ya Simba kwa bao 1-0 wakishuka nafasi ya 12 kwa sawa na wapinzani hao.

Maxime alisema matokeo hayo yalikuwa bora kwao na walihitaji kushinda kwa idadi kubwa ya mabao na licha ya straika kufanya kazi nzuri, lakini tatizo lilikuwa kwa mabeki waliokubali kufungwa.

Alisema kutokana na hatua hiyo wanaenda kujipanga upya kuhakikisha mchezo ujao dhidi ya Geita Gold wanaendeleza ushindi wenye mambo mengi lakini kutoruhusu wavu wao kutikiswa.

“Bado tunahitaji ushindi zaidi wenye idadi kubwa ya mabao, niwapongeze vijana walipambana japokuwa walipoteza umakini eneo la beki, tunaenda kusahihisha makosa ili mechi ijayo na Geita Gold tufanye kweli,” alisema Maxime.

Kocha huyo aliongeza, bado timu hiyo haipo sehemu nzuri na namna ya kuondoka nafasi za chini ni kuendelea kupambana kila mechi bila kujali nyumbani au ugenini ili kufikia malengo.

Ihefu haikuwa na mwanzo mzuri msimu huu hadi kuwafanya mabosi wa timu hiyo kufanya mabadiliko kwenye benchi la ufundi wakimtoa Zuberi Katwila na kumpa majukumu Maxime ambaye ameanza kibabe.

Chanzo: Mwanaspoti