Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao yote manne ya Azam FC vs Kitayosce yanahesabika

Kitayosce Azam Mabao yote manne ya Azam FC vs Kitayosce yanahesabika

Thu, 17 Aug 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Bodi ya Ligi Kuu ya Soka Tanzania Bara imesema kuwa mabao yote yaliyofungwa na Azam FC katika mchezo wao wa jana dhidi ya Kitayosce FC (Tabora United) yanahesabika licha ya mchezo huo kuvunjika.

Hayo yamesemwa na Ofisa Habari Bodi ya Ligi, Karim Boimanda wakati akihojiwa na Azam TV mara baada ya kuvunjika kwa mchezo huo kutokana na wachezaji wa Kitayosce kubaki sita pekee uwanjani huku wawili wakiumia.

Awali Kitayosce iliingia uwanjani na wachezaji nane tu jambo lililoibua maswali lakini hata hao nane hawakumaliza mchezo wote kwani wawili waliumia na kubaki sita jambo lililomlazimu mwamuzi kuvunja mchezo huo kwa mujibu wa kanuni.

“Mwamuzi kumaliza mchezo ni jambo la kikanuni, Kitayocse wakati mechi inaanza walikuwa na wachezaji 8 kiwanjani, kikanuni hapa mechi inachezwa maana kanuni inaelekeza ili mechi ichezwe lazima idadi ya wachezaji iwe kuanzia 8 na sio chini ya idadi hiyo, baada ya mchezo kuanza wachezaji wawili wa Kitayocse wakapata majeraha na kufanya wabakie 6 kiwanjani, kikanuni hapa mchezo hauwezi kuendelea.

"Kama Azam FC wangekuwa hawajafunga mabao wangepewa ushindi wa mabao matatu na pointi tatu kwa kuwa mpaka mchezo unaenda kumalizika kwa dakika zile tayari Azam FC ilikuwa imefunga mabao 4-0, hivyo mabao yao manne na pointi zao tatu zinabakia kama zilivyo.

"Magoli manne ambayo yamefungwa na Azam FC dhidi ya Kitayoce FC [Feitoto magoli matatu na Dube goli moja] yanahesabika kuwa magoli halali na hata kwenye msimamo wa Ligi utakaotolewa utayajumuisha.

"Mchezo umemalizika wakati Azam inaongoza kwa magoli manne, kikanuni magoli yanabaki kama yalivyo lakini endapo Azam ingekuwa imefunga magoli pungufu ya matatu ingepewa alama tatu na magoli matatu.

"Ndio maana hata baada ya mchezo kumalizwa Feitoto amekabidhiwa mpira kama ambavyo kanuni inaelekeza mchezaji atakaefunga magoli matatu atakabidhiwa mpira mara baada ya mchezo kumalizika.

“Kitayosce FC ilianza mechi dhidi ya Azam ikiwa na wachezaji nane [8], Bodi ya Ligi tulipokea uthibitisho kutoka TFF kuwa wachezaji nane [8] tu wa Kitayosce ndio wanastahili kucheza mechi ya Ligi.

“Kikanuni inaruhusiwa timu kucheza ikiwa na wacheza nane [8]. Kanuni inaeleza timu itaruhusiwa kucheza ikiwa na wachezaji wasiozidi 11 na wasiopungua saba [7].

“Kanuni hizohizo pia zinaeleza, endapo itakapotokea wale wachezaji wasiopungua saba mmoja wapo au zaidi akashindwa kuendelea na mchezo kwa maana wakapungua saba mchezo huo utamalizwa/utavunjwa.

“Timu ambayo wachezaji wake wametimia uwanjani itapewa ushindi [alama tatu na magoli matatu] lakini kama ilikuwa imefunga magoli zaidi ya matatu, magoli yaliyofungwa yatasimama hivyohivyo,” amesema Karim Boimanda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live
Related Articles: