Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao yaacha kilio, kicheko Ligi Kuu

Mbao FcKDSCFL 1 Mabao yaacha kilio, kicheko Ligi Kuu

Mon, 27 Jul 2020 Chanzo: mwanaspoti.co.tz

By Charles AbelWAKATI pazia la Ligi Kuu Bara 2019/20 likifungwa rasmi jana Jumapili, mabao yamegeuka lulu kwa kuamua hatima ya timu za kubaki kwenye ligi, kucheza hatua ya mchujo (play-off) na zile za kushuka daraja.

Tofauti na misimu mingine ambayo pointi ndizo zilikuwa zina nguvu katika kuamua hatima ya timu mbalimbali katika ligi, mambo yamekuwa tofauti msimu huu ambapo licha ya timu nne kulingana pointi, baadhi zimejikuta zikishuka daraja, kubaki kwenye ligi na kucheza mchujo licha ya kuwa na pointi sawa na nyingine.

Ushindi wa mabao 2-1 nyumbani dhidi ya Ruvu Shooting uliiokoa Mtibwa Sugar na kuiwezesha kubaki Ligi Kuu licha ya kulingana pointi na timu za Alliance, Mbeya City na Mbao.

Mtibwa Sugar ambayo baada ya ushindi huo imefikisha pointi 45, imebakia kwa kubebwa na utofauti mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kulinganisha na wenzake ambapo imepachika mabao 30 na kuruhusu nyavu zake kutikiswa mara 34.

Timu nyingine iliyoweza kunusurika katika mechi ya mwisho ni Mwadui FC ambayo ushindi wake wa mabao 2-1 dhidi ya Kagera Sugar, umewafanya wafikishe pointi 47 ambazo zimewaacha salama.

Lakini haikuwa Mtibwa tu iliyookolewa na utofauti mzuri wa mabao ya kufunga na kufungwa kwani pia Mbao na Mbeya City licha ya kusota mkiani mwa msimamo wa ligi kwa muda mrefu, zimemaliza kwa ahueni angalau ya kucheza mechi za mchujo dhidi ya timu za Ligi Daraja la Kwanza (FDL) baada ya kupata ushindi katika mechi zao.

Chanzo: mwanaspoti.co.tz