Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao ya mguu wa kushoto, mateso kwa makipa

Left Footer Mabao ya mguu wa kushoto, mateso kwa makipa

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakati washambuliaji wanaotumia miguu ya kushoto wanaona raha, ipo tofauti kwa makipa baadhi ambao wamesema wanafanya kazi kubwa ya kuwadhibiti.

Bodi ya Ligi imetoa idadi ya wachezaji waliofunga mabao kutumia mguu wa kushoto, huku kiungo mshambuliaji Aziz Ki akiwa kinara wa mabao manane kati ya 10 aliyofunga.

Wachezaji wengine waliofunga ni Gibril Sillah wa Azam FC (mabao matatu), Adam Adam wa Mashujaa (mabao 3), Moses Phiri na Clatous Chama wa Simba (mabao mawili), Maxi Nzengeli wa Yanga (mabao mawili), Emmanuel Martin wa Dodoma Jiji (mabao 2) na Edwin Balua wa Prisons (mabao mawili).

Washambuliaji hao, wamezungumza na Mwanaspoti kwa nyakati tofauti, akiianza Balua wa Prisons anayehusishwa kusaini Simba amesema "Huwa najisikia raha zaidi ninapotumia mguu wa kushoto, tofauti na mguu wa kulia, pia nafanya sana mazoezi kutumia mguu huo."

Kwa upande wa Adam wa Mashujaa amesema "Mguu wa kushoto unahitaji ufundi zaidi, lakini mara nyingi makipa wanakuwa hawajajiandaa, jambo linalonipa raha sana."

Mchezaji mwingine aliyezungumzia hilo ni staa wa zamani wa Yanga, Emmanuel Martin amesema "Kufunga na mguu wa kushoto kunahitaji akili zaidi, pale kipa anapodhani unatoa pasi ndio muda unaotumia kufunga."

Kipa wa KMC, Wilbol Maseke amesimulia bao alilofungwa na Ki"Alikuwa kama anataka kupiga shuti kali, akapunguza kasi akafunga kutumia mguu wa kushoto, ila mastaa ambao ni hatari zaidi pengine kuliko Ki ni Sillah, Luis Miquissone wa Simba ni vile hajapata nafasi ya kucheza sana na Tepsi Evance wa KMC.

Ameongeza "Wachezaji hao siyo lazima wakufunge kwani utumiaji wao wa miguu hiyo, kama wakikabwa wanawapa wenzao nafasi ya kufunga."

Mtazamo wake haujatofautiana sana na wa kipa wa Namungo FC, Deogratius Munishi 'Dida' ambaye amesema "Wanaotumia mguu wa kushoto wana ufundi mwingi, inahitaji akili kubwa kuwakaba na kujua wanapokuwa na mpira mguu wanataka kufanya kitu gani."

Chanzo: Mwanaspoti