Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao ya mapema zaidi Ligi Kuu

Morisson Benard Sore Bernard Morrison

Fri, 21 Oct 2022 Chanzo: Mwanaspoti

Ligi Kuu Bara ilipofikia hadi sasa zipo timu zilizocheza raundi tano kama Simba, Yanga, Namungo na Singida Big Stars, huku zikiwepo zilizocheza mechi sita na nyingine saba, katika michezo hiyo, yamepatikana mabao yalifungwa mapema zaidi.

Licha ya tofauti hizo lakini haiwazuii wachezaji kupachika mabao ya dakika za mapema zaidi.

Makala hii inakuchambulia baadhi ya wachezaji waliofunga mabao dakika za mapema kuanzia dakika ya kwanza hadi ya tano kwenye viwanja mbalimbali msimu huu (2022/23).

NICKSON KIBABAGE - MTIBWA SUGAR

Beki wa Mtibwa Sugar, Nickson Kibabage ni kati ya wafungaji wa mabao ya mapema (dakika pili), alifunga dhidi ya Mbeya City, mchezo uliopigwa Uwanja wa Manungu, Februari 10 na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Kibabage alipokea pasi ya George Chota, aliyetengewa mpira na James Kotei hivyo akawasoma mabeki wa Mbeya City na kuona mpenyo wa kuupeleka mpira kambani.

ISMAIL MGUNDA - PRISONS

Mchezaji wa Tanzania Prisons, Ismail Mgunda alifunga bao la penalti dakika ya pili dhidi ya Dodoma Jiji, kipa Aron Kalambo badala ya kuokoa hatari akajikuta amegongana na Khamis Mcha, ikatafsiriwa ni madhambi, jambo lililowapa wapinzani wao faida ya bao la mapema.

Mchezo huo ulimalizika kwa Prisons kushinda mabao 2-1 dhidi ya wenyeji Dodoma Jiji, Ulipigwa Uwanja wa Liti uliopo Singida, Agosti 20.

MOSES PHIRI - SIMBA

Straika wa Simba, Moses Phiri ambaye ana mabao manne Ligi Kuu Bara, alifunga bao la mapema (dakika ya tatu), Baraka Majogoro wa KMC, alipoteza mpira ukamkuta Mzambia huyo, akampunguza beki mmoja na kupiga shuti nyavuni, mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Benjamin Mkapa, Septemba 7 na ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

ALLY KIPEMBA - POLISI TANZANIA

Agosti 21,mchezaji wa Polisi Tanzania, Ally Kipemba alifunga bao la mapema (dakika ya 2) dhidi ya KMC, mchezo ulipigwa Agosti 21 Uwanja Sheikh Amri Abeid, Arusha na ulimalizika kwa sare ya mabao 2-2.

BERNARD MORRISON - YANGA

Winga wa Yanga, Bernard Morrison alifunga bao la mapema (dakika ya nne), winga huyo asiyeishiwa na vituko kila siku alitengenezewa pasi na Jesus Moloko wakicheza dhidi ya Coastal Union ya Tanga, ulipigwa Agosti 20 Uwanja Sheikh Amri Abeid, Arusha ukimalizika kwa Wanajangwani kufunga mabao 2-0.

MATTEO ANTONY - KMC

Straika wa KMC anayemiliki mabao manne kwenye Ligi Kuu, alifunga bao la mapema (dakika ya tatu) dhidi ya Ihefu, timu yake ikishinda 2-1, mchezo uliopigwa Uwanja wa Uhuru, Septemba 20.

“Faida ya kufunga bao la mapema ni kupunguza presha ya wapinzani inategemeana na walivyopokea, pia changamoto ni kuhakikisha unalinda bao na kuongeza ukikutana na timu ambayo inakuwa na uwezo wa kusawazisha,” anasema.

SIXTUS SABILO -MBEYA CITY

Sabilo aliye na mabao matatu Ligi Kuu, alifunga bao dakika ya nne dhidi ya Ihefu, mchezo huo ukimalizika kwa sare ya 1-1, ulipigwa Uwanja wa Sokoine, Oktoba 8.

“Ni vizuri kufanya mahesabu ya mapema, ingawa kazi inakuwa ni kulinda bao na kuongeza lingine ili timu kupata ushindi, ila siyo rahisi kwani kuna wakati wapinzani wanaweza wakasawazisha,” anasema.

Chanzo: Mwanaspoti