Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabao 10 yaliyowekwa kimiani baada ya kupigwa pasi nyingi

Pasi Nyingi Mabao 10 yaliyowekwa kimiani baada ya kupigwa pasi nyingi

Fri, 6 Oct 2023 Chanzo: Mwanaspoti

Hivi kuna kitu kitamu kukitazama kwenye soka zaidi ya pasi nyingi za gonga kisha bao likafungwa?

Kipi, kufunga bao la shuti la mita 30? Asikwambie mtu, kwenye Ligi Kuu England yamefungwa mabao ya kila aina, yakiwamo ya mchezaji kubinuka ‘tick-tack’, lakini haya ndiyo yale 10 matata kabisa yaliyowekwa kimiani baada ya kupigwa pasi nyingi zilizovutia mashabiki.

Gervinho vs Wigan - (pasi 33)

Chini ya Arsene Wenger, Arsenal walijulikana kwa pasi zao nyingi, za kumiminika na mtindo wao wa uchezaji wa kumiliki mpira mwishoni mwa miaka ya 2000 na 2010, hivyo haishangazi kuona The Gunners ikiwamo kwenye orodha hii. Wachezaji wa Arsenal walifanya kazi nzuri sana katika mechi hiyo iliyoanza kwa faulo iliyotokana na mpira kuchezwa kwa pasi fupi fupi za haraka haraka kabla ya kuingia ndani ya eneo la Wigan Athletic.

Robin van Persie alimpasia mpira Gervinho ikiwa ni pasi ya 33 na ya mwisho, kabla ya mchezaji huyo wa zamani wa kimataifa wa Ivory Coast kufunga, na hivyo kuhitimisha juhudi za timu na kuwapa The Gunners uongozi wa mabao 3-0.

Luis Diaz vs Norwich - (pasi 34)

Liverpool siku zote inafurahia mafanikio kila inapocheza dhidi ya Norwich City. Tukirejea enzi za Luis Suarez katika kipindi ambacho aliwanyayasa sana Norwich, walifunga mabao mazuri dhidi ya timu hiyo. Hata bao la Luis Diaz halikuwa tofauti kwani winga huyo alifunga bao zuri kwa timu yake ya Liverpool zikiwa zimepigwa pasi 34 hadi bao kufungwa. Bao hilo liliundwa na pasi fupi fupi pia tulishuhudia kipa Allison akirudishiwa mpira nyuma kwa pasi hivyo kuhusika katika pasi zilizozaa bao hilo. Pasi ya mwisho, iliichana safu ya ulinzi ya Norwich huku Diaz akikimbia kwa kasi na kufunga.

Mesut Ozil vs Newcastle - pasi 35

Alijulikana kwa uwezo wake mkubwa wa kucheza soka. Kiungo huyo aliyestaafu soka kwa sasa alifunga bao kali dhidi ya Newcastle mwaka 2020 wakati anakipiga Arsenal. Bao hilo lilitokana na pasi 35 kupigwa hadi mpira kuingia nyavuni na lilifungwa katika dakika ya 90 ya mtanange huo wa Ligi Kuu England. Bao hilo lilikuwa la nne kwa upande wa Arsenal.

Ashley Young vs Blackburn Rovers - pasi 37

Chini ya Sir Alex Ferguson, Manchester United ilikuwa moto wa kuotea mbali, na wachezaji walipambana na kupata mafanikio. Sio tu kutokana na uwezo binafsi wa mchezaji mfano mzuri bao alilofunga Ashley Young dhidi ya Blackburn mwaka 2012. Bao la kwanza liliwekwa kimiani na Antonio Valencia, lakini bao alilofunga Young lilikuwa kali zaidi kwa sababu zilipigwa pasi 37 hadi mpira kumfikia na kuuweka kambani. Mwishowe Man United ikaibuka na ushindi wa mabao 2-1. Lilikuwa bao bora katika mwaka wa mwisho wa Ferguson.

Morgan Schneiderlin vs Newcastle - pasi 40

Miaka ya nyuma, Southampton ilikuwa moja ya timu nzuri Ligi Kuu England. Wachezaji kama Victor Wanyama, James Ward-Prowse, Toby Alderweireld na Morgan Schneiderlin walikuwepo katika timu, walikuwa moto kwelikweli kwani iliibamiza Newcastle United mabao 4-0 mwaka 2014. Baada ya mabao mawili yaliyofungwa na Graziano Pelle na Jack Cork, zilipigwa pasi 40 kwanza ndipo Schneiderlin alipofunga bao lake katika ushindi huo.

Sergio Aguero vs Everton - pasi 42

Kuingia tano bora katika msimamo, unahitaji juhudi kama za Sergio Aguero dhidi ya Everton. Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester City alifunga mabao ya kukumbukwa katika historia ya Lig Kuu England. Lakini mara chache alifunga bao moja ambalo lilionyesha muuganiko wa ajabu kama alivyofanya dhidi ya Everton mwaka 2021 kwani zilipigwa pasi 42 kwanza na kufunga kwa kichwa Man City ikiibuka na ushindi wa mabao 5-0.

Ilkay Gundogan vs Manchester United - pasi 44

Kiungo huyo wa zamani wa Manchester City anayekipiga Barcelona kwa sasa alifunga bao kali dhidi ya Manchester United mwaka 2018. Pasi zilipigwa 44 hadi bao kupatikana kwani Gundogun alimpita David de Gea na kuipa ushindi timu yake, mashetani wekundu wakiwa tayari washachezea mabao 2-1 kabla ya Gundogan kufunga bao hilo la tatu.

Juan Mata vs Southampton - pasi 45

Bao la Mata alilofunga lilikuwa la kipekee dhidi ya Southampton mwaka 2015, kiungo huyo wa zamani wa Man United alifunga bao la tatu baada ya kupigwa pasi 45 kabla mpira kumkuta Mata.

Kiungo huyo alikuwa hana tatizo kabisa kwenye umaliziaji wa mpira huku wakionyesha soka safi kwa mara kwanza tangu Sir Alex Ferguson alipoondoka miaka miwili iliyotangulia. Bao la Mata lilikamilisha mchezo huo kwa ushindi wa mabao 3-2.

Phil Foden vs Nottingham Forest - pasi

Baada ya kuupata mpira bao Phil Foden dhidi ya Nottingham Forest lilikuwa kali Pep Guardiola akitawala mchezo huo. Man City ilipiga pasi 46 kabla ya kiungo huyo wa kimataifa kuwekewa pasi na Kyle Walker na kudumbukiza mpira nyavuni, Man City ikiibuka na ushindi wa mabao 2-0 katika mechi hiyo ya Ligi Kuu England.

Nacer Chadli vs Queens Park Rangers - pasi 48

Chadli alifunga bao zuri dhidi ya Queens Park Rangers mwaka 2014 ambalo lilitokana na pasi nyingi kupigwa. Jumla ya pasi 48 zilipigwa wakati bao hilo likipatikana. Tottenham Hotspur iliibuka na ushindi wa mabao 4-0 lakini mashabiki walipagawa zaidi na bao la Chadli. Chadli alikipiga Spurs kwa muda wa miaka mitatu kabla ya kujiunga na West Bromwich Albion mwaka 2016.

Chanzo: Mwanaspoti