Kila mchezaji anapenda kupata matokeo mazuri kwa ajili ya timu yake ipo hivyo. Sio Yanga, Singida Fountain Gate mpaka Kagera Sugar.
Hata Namungo pia wanafanya maandalizi kwa ajili ya kuona wanapata kile kilicho bora uwanjani.
Kila shabiki anapenda kuona timu yake inapata matokeo mazuri baada ya dakika 90. Kwa namna yoyote kinachotakiwa kwa wakati huu ni umakini kwa kilasekta kuanzia kwa mashabiki mpaka wachezaji kutimiza majukumu yao.
Wachezaji wanatambua baada ya ratiba ya ligi kuwekwa wazi kinachofuata ni kuvuja jasho la kusaka ushindi. Ushindi unatafutwa kwa mbinu na wachezaji kutumia makosa ya wapinzani.
Kuanzia kwenye Ngao ya Jamii hapo ni muhimu wachezaji kutimiza majukumu yao kwa umakini. Kupata matokeo chanya hakutokei kwa bahati mbaya.
Ni Yanga, Simba, Azam FC na Singida Fountain Gate hizi zinashiriki Ngao ya Jamii inayarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.
Nidhamu ya wachezaji kwa kufuata kile ambacho walipewa wakiwa uwanja wa mazoezi na kutumia nafasi watakazozipata uwanjani.
Mpira ni mchezo wa wazi kila kila kitakachotokea kitaonekana kwa mashabiki na benchi la ufundi litapata muda wa kujua ni wapi ambapo wanapaswa kuboresha.
Maboresho ambayo yatafanyika kwenye mchezo mmoja ni lazima yaendelee kufanyiwa kazi kwa mechi zinazofuata ili timu kuzidi kuwa imara.
Mashabiki wekeni kando tofauti zenu zitakazosababisha ugomvi baada na kabla ya mchezo bali kuwa bega kwa bega na timu zenu zinapopata matokeo na zinapokosa matokeo. Hakuna mwalimu anayepeleka timu uwanjani akiwa anafikiria kushindwa.
Kama mwalimu hafikirii kushindwa basi na mashabiki nao wanapenda kuona timu inapata ushindi. Msimu mpya ukawe na mabadiliko kila idara.