Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Mabadiliko manne yaliyofanywa na Simba

Mabadiliko Pic Data Simba yafanya mabadiliko manne

Thu, 28 Oct 2021 Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz

KIKOSI cha Simba leo kinashuka dimbani dhidi ya  Polisi Tanzania huku kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo, Thierry Hitimana akija kivingine akifanya mabadiliko kwenye kikosi hicho.

Hitimana amefanya mabadiliko kwenye beki ya kati akiamza Joash Onyango na eneo la ushambuliaji ameanza na Meddie Kagere ambaye hakuwa na namba kikosi cha kwanza cha Diddie Gomes.

Nyota wengine waliopewa nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mchezo wa leo ni Kibu Denis na Erasto Nyoni.

Kikosi cha Simba kinachotarajia kukipiga dhidi ya Polisi Tanzania kipa ni Aishi Manula mabeki ni Shomari Kapombe, Mohammed Hussein, Onyango, Enock Inonga,

Wakati nafasi ya kiungo ameanza na mkongwe Etasto Nyoni na Sadio Kanout huku safu ya ushambuliaji iliongozwa na Meddie Kagere ambaye amekaa nje kwa muda atasaidiana na Rally Bwalya wakati mawinga ni Kibu Denis na Hassan Dillunga.

Chanzo: www.mwanaspoti.co.tz