FC Barcelona haijakata tamaa juu ya uwezekano wa kumbakisha Kocha Xavier Hernández Creus, hata hivyo si wachezaji wote kwenye kikosi hicho wanaamini anafaa kusalia baada ya msimu kumalizika.
Rais wa klabu hiyo Joan Laporta amebainisha wazi kuwa angependa kuona Xavi anabaki katika klabu hiyo na yuko tayari kumpa kocha huyo raia wa Hispania mkataba mpya.
Lakini, katika chumba cha kubadilishia nguo, maoni haya hayakubaliwi na wachezaji wote, kwani wanaamini Xavi amefanya kila awezalo.
Inasemekana baadhi ya wachezaji kikosi hicho wanatamani kuwa na kocha mpya na mwenye uzoefu zaidi. Wachezaji wakongwe, Sergi Roberto na Robert Lewandowski wameelezea masikitiko yao juu ya kuondoka kwake.
Hata hivyo, ripoti za Desemba zilidai kuwa Lewandowski, Ikay Gundogan, Frenkie de Jong na Marc-Andre ter Stegen hawakufurahishwa kabisa na mtindo wake wa ukocha.
Baada ya maisha marefu kama mchezaji aliyevalia jezi ya Barcelona, Xavi aliajiriwa kama kocha mkuu mwaka wa 2021. Sasa, inaonekana huenda safari yake inakaribia kuisha, huku akitafuta kuondoka kwa wababe hao wa Katalunya.
Mfarakano unaweza kutokea kwenye chumba cha kubadilishia nguo, lakini watu kwenye chumba cha mikutano hawana nia ya kumuongezea muda Xavi.
Laporta na makamu wa rais Rafa Yuste ndio mashabiki wake wakubwa na wanafahamu kuwa kutafuta mbadala wa Xavi litakuwa swali gumu na wana nia ya kumshawishi kubatilisha kujiuzulu kwake.