Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu yanayoendelea kwa vigogo Afcon

Morocco AFCON Out Maajabu yanayoendelea kwa vigogo Afcon

Thu, 1 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Fainali za mataifa ya Afrika zinaendelea nchini Ivory Coast ambapo moja kati ya mambo yaliyoibuka ni kutolewa kwa vigogo wengi kuanzia hatua ya makundi hadi 16 bora. Mbaya zaidi timu zote tano zilizoiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia nchini Qatar 2022 zimeshindwa kufika robo fainali ya Afcon mwaka huu. Hapa tunakuletea timu tano zilizoiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia 2022 zilizoshindwa kufuzu robo fainali.

Senegal Wakiwa mabingwa watetezi wa michuano ya Afcon, Senegal waliingia wakiwa na matarajio makubwa. Timu hiyo ilikuwa na mastaa kibao ikiwa pamoja na Sadio Mane anayeichezea Al Nassr ya Saudi Arabia.

Pia wana mastaa kama Nicolas Jackson (Chelsea), Abdallah Sima (Rangers), Iliman Ndiaye, Ismaila Sarr (Marseille), Drissa Gana Gueye (Everton) na Youssouf Sabaly anayeichezea Real Betis. Hata hivyo, safari ilifikia kikomo baada ya kutolewa na wenyeji, Ivory Coast kwa mikwaju ya penalti.

Morocco

Timu hiyo iliyotinga nusu fainali katika michuano iliyopita ya Kombe la Dunia iliingia katika fainali za Afcon ikiwa na matumaini ya kufanya makubwa. Hata hivyo, safari ilikatizwa na Afrika Kusini.

Morocco ina mastaa wengi wakiwamo Achraf Hakimi anayeichezea PSG, Abdelkabir Abqar (Deportivo Alavés), Nayef Aguerd (West Ham), Chadi Riad (Betis), Noussair Mazraoui (Bayern Munich), Selim Amallah (Valencia), Amir Richardson (Stade de Reims), Oussama El Azzouzi (Bologna FC), Sofyan Amrabat (Manchester United), Hakim Ziyech (Galatasaray) na Youssef En-Nesyri waa Sevilla.

Ilipata matokeo mazuri katika kundi F baada ya kukusanya pointi saba kwa kushinda mara mbili ikianza kushinda 3-0 dhidi ya Tanzania na 1-0 dhidi ya Zambia kisha ikatoka sare ya bao 1-1 na DR Congo.

Ghana Hawa walikuwa kwenye kundi lililojumuisha Cape Verde, Misri, na Msumbiji. 'Black Stars' walishindwa kutinga 16 bora baada ya kumaliza nafasi ya tatu wakiwa na pointi mbili. Matokeo hayo yalionekana kuwashangaza watu wengi kwa sababu Ghana imetoka kucheza fainali za Kombe la Dunia. Pia ni mabingwa wa taji hilo 1982 ambapo mashindano yalifanyika Libya. Imepita miaka 40 tangu taifa hilo lilipochukua taji hilo kwa mara ya mwisho.

Cameroon Ingawa ilifuzu hatua ya 16 bora, Cameroon ilishindwa kufuzu katika robo fainali baada ya kuchapwa mabao 2-0 na Nigeria. Cameroon ambao waliandaa mashindano yaliyopita walishindwa kurudia maajabu ya mwaka 2017 walipobeba ubingwa.

unisia Hawa walimaliza mkiani kwenye kundi wakiwa na pointi mbili na ilikuwa moja kati ya nchi zilizoiwakilisha Afrika kwenye Kombe la Dunia. Kushindwa kwao kumezua maswali kuhusu hali ya soka la Tunisia ambalo siku hadi siku linaonekana kushuka.

MSIKIE MAYAY Mkurugenzi wa Maendeleo ya Michezo Tanzania, Ally Mayay amesema kinachoendelea katika fainali za Afcon kinaonyesha jinsi nchi nyingi zilivyowekeza kwenye soka. Mayay ametoa mfano wa Cape Verde ambao walifanikiwa kufuzu hatua ya mtoano ya mashindano na kuduwaza watu wengi.

"Ukiichambua timu ya taifa ya Cape Verde iliyocheza dhidi ya Tanzania miaka michache iliyopita unaweza kuona jinsi timu hiyo ilivyopata mafanikio baada ya kubadili fikra za mchezo na kuwekeza zaidi katika maendeleo ya vijana," amesema.

“Nani alifikiria kuhusu Cape Verde, Guinea na Angola kwamba wangefika hatua hii? Nani pia alifikiria kuhusu Misri, Morocco, Algeria, Cameroon, Ghana, Tunisia na Senegal kwamba wangetolewa katika hatua hii na wengine katika hatua ya kundi? Kuna mabadiliko chanya katika soka la Afrika ambayo Tanzania inaelekea pia."

Chanzo: Mwanaspoti