Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu ya soka usiyoyajua, utashangaa

Harry Maguire Player Mambo muhimu usiyoyajua kuhusu soka, utashangaa

Thu, 5 Sep 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mtoto wa Cristiano Ronaldo, Ronaldo Junior na mtoto wa Lionel Messi, Thiago Andreas Messi wanapishana siku (869) za kuzaliwa, sawa na umri wanaopishana baba zao Lionel Messi na Cristiano Ronaldo.

➜ Kiungo fundi, Kevin De Bruyne hajawahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi England Premier league lakini ametwaa tuzo ya mchezaji bora wa msimu mara mbili.

➜ Kocha Jose Mourinho hakuwahi kupoteza mechi nyumbani kwa muda wa miaka (9) sawa na Michezo (150) akiwa kocha wa FC Porto, Chelsea, Inter Milan na Real Madrid kuanzia 16 March 2002 hadi 2 April 2011.

➜ Beki wa kati, John Terry amefunga magoli mengi (EPL) akiwa Chelsea (68 ⚽) kumzidi fundi Andres Iniesta aliyefunga mabao (35) tu La Liga akiwa FC Barcelona.

➜ Mark Hughes na Cole Palmer ndio wachezaji (2) pekee ambao walicheza mechi (2) tofauti (rasmi) ndani ya siku moja.

• Asubuhi Mark Hughes aliitumikia timu ya Taifa ya Wales na Alasili akaitumikia klabu ya Bayern Munich.

• Cole Palmer aliitumikia klabu ya Manchester city (Senior team) Alasili na Jioni akafunga Hattrick akiwa team (B U23).

➜ 2016 Cristiano Ronaldo alitwaa makombe (4) kuzidi idadi ya mechi alizopoteza (3).

➜ Lionel Messi ndiye mchezaji pekee aliyetwaa tuzo ya Ballon d'or katika Decades | Miongo (3) tofauti.

➜ Layvin Kurzawa ana hat-trick nyingi UEFA champions league kuwazidi Xavi, Zidane, Kroos na Suarez kwa pamoja.

➜ Raphinha ana hatricks nyingi La liga kumzidi Ronaldinho Gaucho!.

➜ Neymar alikuwa mchezaji wa kwanza wa FC Barcelona kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwezi La liga (November 2015).

➜ Klabu ya Nottingham Forest imetwaa makombe mengi ya UEFA Champions kuliko klabu za Manchester City, Arsenal, Atletico Madrid na Tottenham kwa pamoja.

➜ Klabu ya Chelsea ilishashuka daraja mara (6), mara nyingi kuliko idadi ya makombe ya (EPL) waliyotwaa (5).

➜ Harry Maguire ndiye mchezaji pekee England aliyewahi kushuka daraja mara mbili katika msimu mmoja.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live