Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu ya mabao manne ya Dube Simba

Dube Kofia.jpeg Prince Dube

Sun, 11 Feb 2024 Chanzo: Mwanaspoti

Wakatic Azam FC ikiifikisha Simba mechi ya nne bila ushindi, mshambuliaji Prince Dube ameweka rekodi kivyake dhidi ya Wekundu hao wa Msimbazi. Dube amefikisha mabao manne akiwafunga Simba kwenye mechi nne tofauti akiwa ndiye staa wa Azam aliyewafunga Wekundu wa Msimbazi mabao mengi mpaka sasa.

Rekodi hiyo ya Dube alianza kuitengeneza kuanzia Oktoba 27, 2022 akiifungia Azam bao pekee la ushindi kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba ambalo alilitupia katika dakika ya 35 akitumia vyema pasi ya kiungo James Akaminko.

Bao la pili dhidi ya Simba alifunga Februari 21,2023 akitumia dakika mbili tangu kuanza kwa mchezo akipokea tena pasi ya Akaminko kisha baadaye Wekundu kusawazisha jioni dakika ya 90 kupitia kwa Kibu Denis na mchezo kumalizika kwa bao 1-1.

Kisha, bao la tatu la Mzimbabwe huyo dhidi ya Simba lilikuja kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho katika wa nusu fainali akiingia kutoka benchi dakika ya 69 akafunga bao la ushindi dakika ya 75 akipokea pasi ya kichwa ya winga Ayoub Lyanga.

Bao la nne ndio la jana alilofunga katika Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza kwenye mechi ya ligi lililokuja dakika ya 14 akimtungua kipa Ayoub Lakred akitumia pasi ya beki wa kushoto wa Azam FC, Pascal Msindo.

Rekodi nyingine kwa Dube ndani ya mabao hayo ni kwamba mshambuliaji huyo kila alipowafunga Simba, Wekundu hao hawakuwahi kuondoka na ushindi ambapo kama sio kupoteza basi timu hiyo ililazimishwa sare.

MBIO AKILI MTAJI WAKE

Katika mechi ambazo Dube amewafunga Simba amekuwa akionyesha ubora wa kuwazidi akili ya uamuzi mabeki wa Simba, kasi na hata hesabu za kujua kuwakimbia mabeki wa Wekundu hao.

DABO AMZUNGUMZIA

Kocha wa Azam akizungumzia rekodi hiyo ya Dube, alisema mshambuliaji huyo ameendelea kuimarika na kuwa na makali zaidi ambapo endapo ataendelea kuwa sawa kiafya anaweza kuwa na rekodi nyingi nzuri zaidi.

“Huyu (Dube) ni mshambuliaji mwenye makali na anaendelea kuwa bora tofauti na nilivyomkuta. Tunapokuwa na Dube uwanjani timu inakuwa na nguvu kubwa kule mbele. Kama akiendelea kuwa sawa kiafya anaweza kuwa na rekodi kubwa zaidi ya hii,” alisema Dabo.

Chanzo: Mwanaspoti
Related Articles: