Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu ya Morisson, Mzamiru yaibeba Simba kwa Mkapa

Maajabu Mzamiru Kiungo wa Simba, Mzamiru Yassin akishangilia goli lake

Wed, 1 Dec 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mabingwa watetezi wa Ligi Kuu Tanzania Bara (NBC Primia Ligi) wametakata kwa ushindi mwembamba wa magoli 2-1 dhidi ya Geita Gold katika Uwanja wa Mkapa Jijini Dar es Salaam.

Winga Peter Banda alikua wa kwanza kuipatia Simba goli kipindi cha kwanza dakika ya tisa ya mchezo akimalizia pasi safi ya Kibu Denis.

Mpaka kipindi cha kwanza kinamalizika Simba walikua mbele kwa goli 1-0.

Kipindi cha pili kilianza kwa Geita Gold kurudi na kasi ya kutafuta goli la kusawazisha na wakatawala sehemu kubwa ya mchezo.

Kocha wa Simba Pablo Martin ilipofika dakika ya 56 akafanya mabadiliko akamtoa Ibrahim Ajibu na kumuingiza Bernard Morrison, kisha akamtoa kiungo Rally Bwalya na kumuingiza Mzamiru Yassin.

Wakati mabadiliko hayo yakifanyika Simba walikua wamepata adhabu ya mpira wa faulo ambapo Morisson alikwenda kupiga lakin alimpasia Mzamiru ambae akapiga mpira kiufundi na kuiandikia Simba goli la pili 57'.

Geita Gold wakacharuka na kufanikiwa kupata bao dakika ya 66 likiwekwa kimiani na Juma Mahadhi.

Kwa ushindi huo Simba wanaendela kukamata nafasi ya pili nyuma ya vinara Yanga wanaoongoza Ligi.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live