Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maajabu! Chama atemwa Timu ya Taifa, Musonda Fresh

Chama Musonda M Maajabu! Chama atemwa Timu ya Taifa, Musonda Fresh

Wed, 22 May 2024 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kiungo wa Simba Clatous Chama ametemwa kwenye kikosi cha timu ya Taifa ya Zambia kitakachocheza mechi mbili za kusaka tiketi ya kucheza Fainali za Kombe la Dunia.

Hata hivyo, kocha wa Zambia Avram Grant amemjumuisha mshambuliaji wa Yanga Kennedy Musonda kwenye kikosi hicho cha wachezaji 27.

Zambia maarufu kwa jina la Chipolopolo itacheza mechi mbili zilizofuatana dhidi ya Morocco na Tanzania zitakazochezwa Juni 7 na 11.

Kwenye kikosi hicho makipa walioitwa ni Charles Kalumba, Lawrence Mulenga, Victor Chabu na Toaster Nsabata.

Wamo mabeki saba, Stopila Sunzu, Chongo Kabaso, Killian Kanguluma, Frank Musonda,Tandi Mwape, Gift Mphande na Luka Banda.

Kocha huyo wa zamani wa Chelsea ya England amewaita viungo 11 wakiwemo Benson Sakala,Miguel Chaiwa, Obina Chisala, Lubambo Musonda, Abraham Siankombo, Kelvin Kapumbu, Emmanuel Banda, Kings Kangwa,Joshua Mutale, Kelvin Kampamba na Gamphani lungu.

Washambuliaji ni Patson Daka, Evanc Kangwa, Kingson Mutandwa, Edward Chilufya na Musonda.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live