Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafisa Habari Yanga wawatungua Maafisa Habari wa Simba

Maafisa Habari Yanga Wawatungua Maafisa Habari Wa Simba.jpeg Maafisa Habari Yanga wawatungua Maafisa Habari wa Simba

Fri, 31 Mar 2023 Chanzo: Bbc

Machi 30, 2023 Waziri wa Habari, Mawasiliano na Teknolojia ya Habari, Mhe. Nape Nnauye (Mb) ameongoza Maafisa Habari katika mchezo wa mpira wa miguu kati ya Maafisa Habari Mashabilki wa Simba na Maafisa Habari Mashabiki wa Yanga uliofanyika katika kiwanja cha Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Mchezo huo umeisha kwa ushindi wa magoli Matatu (3) kwa upande wa Maafisa Habari wa Yanga uku kinara wa Magoli akiwa ni Msemaji Mkuu wa Serikali na Mkurugenzi wa Idara ya Habari Maelezo, Bw. Gerson Msigwa kwa kufunga magoli mawili kati ya matatu yaliyofungwa na timu hiyo huku Maafisa Habari Mashabiki wa Club ya Simba wakitoka na sifuri

Mchezo huo umechezwa baada ya kufungwa kwa Kikao Kazi cha Maafisa Habari, Uhusiano na Mawasiliano Serikali, 2023 kilichofunguliwa Siku ya Jumatatu 27 Machi, 2023 na kufungwa Machi 30, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC).

Chanzo: Bbc