Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafande wamuweka Mayele chini ya ulinzi

Mayele Ruvu Maafande wamuweka Mayele chini ya ulinzi

Mon, 3 Oct 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kinara wa mabao wa Yanga, Fiston Mayele amewekwa chini ya ulinzi na mabeki wa kati wa Ruvu Shooting, Tariq Abed na Frank Nchimbi katika dakika 45 za kipindi cha kwanza.

Licha ya kuwa Mayele alipoteza nafasi ya kuifanya Yanga iende mapumziko ikiwa mbele mwanzoni mwa kipindi cha kwanza kwa kichwa, mabeki hao wanaonekana kumpa upinzani mkali.

Kila ambapo Mayele alikuwa akisogea eneo la hatari la Ruvu Shooting, Nchimbi na Abed walimweka chini ya ulinzi huku wakiondoa krosi za hatari ambazo zilikuwa zikichongwa kutokea pembeni.

Katika dakika 45 za kipindi cha kwanza Yanga imeonekana kutumia zaidi maeneo yao ya pembeni ambako walikuwa wakicheza Tuisila Kisinda na Farid Mussa kusukuma mashambulizi yao.

Vijana wa Boniface Mkwasa wamekana kucheza kwa nidhamu hasa katika kujilinda, nguvu yao inaonekana kuwa ndogo kwenye safu yao ya ushambuliaji ambayo wameanza, Samsoni Joseph, Rashid Juma na Abalkassim Sulleiman.

Shaban Msala katika eneo la kiungo cha Ruvu Shooting ndiye mchezaji ambaye anaonekana kuibeba timu, ni mwepesi wa maamuzi, anaifanya timu kusogea.

Kocha wa Yanga, Nasreddine Nabi anakibarua kizito katika kipindi cha pili kwani ndani ya dakika 45 za kwanza, wapinzani wao wanaonekana kuwa wengi katika eneo lao.

Kitu ambacho kinawafanya mashambuliaji wa Yanga kuwa na wakati mgumu kumfikia kipa wa Ruvu Shooting, Hussein Msalanga.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live