Michezo

Habari

Burudani

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Maafande wa Prisons waiita Simba mezani

Edwin Balua Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Edwine Balua

Thu, 4 Jan 2024 Chanzo: Dar24

Kiungo mshambuliaji wa Tanzania Prisons, Edwine Balua na uongozi wa Maafande hao umesema unawasubiri ofa kutoka kwa Wekundu wa msimba Simba, huku nyota huyo akiweka wazi yupo tayari kwenda popote.

Balua amekuwa na kiwango bora tangu ajiunge na ‘Wajelajela’ hao wa jijini Mbeya misimu miwili sasa akitokea Coastal Union huku akiwa na uhakika wa namba kikosi cha kwanza.

Hivi karibuni tetesi zimekuwa zikisambaa Wekundu hao tayari wametuma ofa kwa nyota huyo ambaye mkataba wake na Prisons unaisha mwisho wa msimu huu na wanahitaji huduma yake.

Balua ambaye aliwahi kuwatungua Wekundu hao mwanzoni mwa msimu huu kwenye kipondo cha 3-1 kwenye Uwanja wa Sokoine, amesema bado hajapokea simu yoyote na kinachoendelea anasikia tu mitandaoni.

“Nipo tayari kucheza popote kwa sababu mchezaji yeyote ndoto zake ni kucheza kwa mafanikio kwenye timu kubwa, hivyo kama ofa itafika tukakubaliana hamna shida,” amesema Balua mtaalanmu wa mipira adhabu.

Meneja wa timu hiyo, Raulian Mpalile alisema, “Waje tu tuzungumze kwa sababu mchezaji bado ana mkataba na timu, tunasikia taarifa hizo ila uongozi bado haujazungumza na hao wanaomtaka, hatuwezi kuzuia chochote mpira ni maisha”

Chanzo: Dar24